Kama ilivyo ada, katika msimu huu wa sikukuu, Multichoice tanzania imetangaza neema kwa watanzania kwa kutoa ofa kabambe kwa wateja wake ambapo kuanzia leo mteja mpya wa DStv ataweza kuunganisha kwa shilingi 79,000 tu hii kikiwa ni vifaa vyote pamoja na kifurushi cha DStv Bomba cha mwezi mzima.

Akizungumzia ofa hiyo, kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Hilda Nakajumo, amesema kuwa Multichoice imekuwa na utamaduni wa miaka nenda rudi wa kuwapa zawadi wateja na watanzania kwa ujumla na kwamba kila ufikapo msimu kama huu DStv huwatunuku wateja wake ili kuwawezesha kufurahia zaidi msimu huu wa sikukuu.

Tunafahamu kuwa msimu huu wa sikukuu familia nyingi zinaungana katika kusherehekea, hivyo DStv imeamua kuwaongezea burudani kwa kutoa ofa hii kabambe. Amesema badala ya mteja mpya kulipa shilingi 98,000 kwa ajili ya kuunganishwa pamoja na kifurushi cha mwezi, sasa watalipa shilingi 79,000 tu na kuunganishwa na DStv pamoja na kifurushi cha Bomba cha mwezi mzima.

“Tunapokuwa nyumbani na familia zetu, watoto wanataka waangalie katuni, sisi kinamama tunapenda kuangalia vipindi kama vile vya mapishi, urembo, na tamthilia, kinababa nao hupenda sana kutazama michezo mbalimbali kama kandanda na kadhalika. Ni kwa msingi huu tumeamua kuwarahisishia burunani hii inayopatikana kutoka DStv” alisema Hilda na kuongeza kuwa wataendelea kutoa ofa kwa wateja wao kila inapihitajika.

Ofa hii ni kwa nchi nzima na itaendelea kwa miezi miwili hadi Januari 15, 2018 Ofa hii kwa wateja wapya inakuja siku chache tu baada ya DStv kuanza kutoa zawadi kwa wateja wake kwa kuwaongezea chaneli za SuperSport kwenye vifurushi vyao punde walipiapo akaunti zao kabla hazijakatika.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: