Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wanaoishi na kufanya shughuli zao za uvuvi Ziwa Victoria, katika kijiji cha Nyang’ombe kilichopo wilayani Rorya, Mkoani Mara.Katika ziara hiyo Naibu Waziri aliambatana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala ikiwa na lengo la udhibiti uhalifu na uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala , akizungumza na wananchi wanaoishi na kufanya shughuli zao za uvuvi Ziwa Victoria katika kijiji cha Nyang’ombe kilichopo wilayani Rorya, mkoani Mara. Lengo la ziara hiyo ni kudhibiti uhalifu na kudhibiti uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.
 Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, akizungumza na wananchi wanaoishi na kufanya shughuli zao za uvuvi Ziwa Victoria katika kijiji cha Nyangombe, kilichopo wilayani Rorya, mkoani Mara. Lengo la ziara hiyo ni kudhibiti uhalifu na kudhibiti uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.
 Mwananchi wa kijiji cha Nyang’ombe akiuliza maswali kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara ya kikazi ambapo naibu waziri aliongozana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, lengo la ziara hiyo ni kukagua udhibiti uhalifu na uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.
Wananchi wakishangilia jambo wakati Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), akizungumza katika mkutano uliofanyika kijiji cha Nyang’ombe ,wilayani Rorya. Naibu Waziri yupo katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua udhibiti uhalifu na uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: