Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dk. Laurent Shirima,akizugumza wakati wa hafla ya utilianaji saini wa mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) leo jijini Dar es Salaam.(kushoto)ni Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’I Issa
Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dk. Laurent Shirima(kulia)pamoja na Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’i Issa wakisaini mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano wanaoshuhudia (kulia )ni Mwanasheria Mwandamizi wa PPRA, Agnes Sayi na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji, Esther Mmbaga.
Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dk. Laurent Shirima, pamoja na wakibadilisha hati za mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watendaji na waandishi wa habari wakiwa katika hafla hiyo.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

MAMLAKA ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), wametiliana saini mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano

Mkataba huo uliosainiwa leo Dar es Salaam, utawezesha PPRA na NEEC kushirikiana kiutendaji ili kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati kushiriki kwenye fursa mbalimbali zinazopatikana katika manunuzi ya umma.

Akizungumza wakati wa hafla ya utilianaji saini mkataba huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dk. Laurent Shirima, lengo linguine ni mamlaka kuhakikisha kigezo mojawapo wakati wa hatua ya tathimini kwenye zabuni za umma cha upendeleo kwa ajasiriamali wadogo na kati kinazigatiwa.

“Pia kila mwaka PPRA na NEEC kufanya tathimini ya pamoja ili kujua namna taasisi nunuzi zinavyotekeleza au kuzingatia ushiriki wa wajasiriamali wadogo na wakati,”alisema Dk. Shirima.

Malengo mengine ni PPRA na NEEC kufanya tafiti za pamoja zitakazo jikita zaidi katika uwezeshaji na ushiriki wa wajasiriamali wadogo na kati kwenye michakato ya manunuzi ya umma.

“Suala la kuwajengea wananchi uwezo wa kupambana na umasikini kwa kushiriki katika shughuli za kiuchumi limekuwa kipaumbele kikubwa cha serikali na hasa ya awamu ya tano.

Ili kufanikisha azma hiyo , serikali imekuwa ikiandaa sera na sheria mbalimbali zinazoweka mazingira mazuri ya wananchi kushiriki na kuitumia fursa za kibiashara,”lifafanua Dk. Shirima.

Alisema moja ya sekta inayotoa fursa kwa wananchi kushiriki kwenye shughuli za kukuza uchumi wan chi ni sekta ya manunuzi ya umma, hivyo wananchi mmojammoja au kwa makundi wakijengewa uwezo wanaweza kuchangamkia fursa zilizopo kwenye sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kushuriki kwenye hatua mbalimbali ya zabuni zinazotolewa na taasisi za umma.

“Ni matuani yetu kwamba wananchi walio katika makundi husika watachangamkia fursa hii ya kujwakwamua kiuchumi na kijamii katika maeneo yao,”alibainisha.

Alisema taasisi za ununuzi, hasa halmshauri zinatarajiwa kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria ili kufanikisha lengo la serikali la kutoa upendelea kwa makundi maalum yamekuwa yanashindwa kunufaika na fursa zilizo katika sekta ya ununuzi wa umma.

Kwa upande wa Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’I Issa, alisema kupitia ushirikiano huo watahakikisha tathimini ya ushiriki wa biashara ndogo na za kati unafanyika katika ukaguzi wa ununuzi wa taasisi za umma.

“Pia taasisi ambazo zitatoa zabuni kwa wafanyabiashara wadogo na wakati kwa kiwango kilichoainishwa katika sheria kwa makundi maalum ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kutambuliwa,”alisema Beng’i.

Alisema utekelezaji wa ushirikiano huo unalenga kuhakikisha biashara, kampuni au vikundi vinavyomilikiwa hasa na wanawake , vijana na watu wenyeulemavu zinapata fursa kushiriki kwenye zabuni za taasisi za umma.

“Hii itasaidia kukuza uchumi wao ili kutekeleza ibara ya 57(e)(vi) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Pia kuwezesha kutathimini ushiriki wa biashara ndogo na za kati ili kupata takwimu sahihi zitakazowezesha serikali kuchukua hatua stahiki za kuwawezesha,”alibainisha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: