Naibu Mkurugenzi wa EngenderHealth Lulu Ng’wanakilala akielezea kuhusu miradi ambayo imekuwa ikifadhiliwa na asasi anayoiongoza. Wakati asasi ya EngenderHealth ikikabidhi vituo vya afya 26 kwa serikali, hafla hiyo imefanyika katika kijiji cha Mwakizega, wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma
Mwakilishi wa Bloomberg Philanthropies Dr Godson Maro akiwasilisha salamu na kuelezea kuhusu asasi anayoiwakilisha.
Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mwanamvua Hoza Mlindoko akimkaribisha mgeni rasmi naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa jamii, Jinsia, Wazee na watoto katika sherehe hiyo ya makabidhiano.
Umati wa wanakijiji waliohudhuria hafla hiyo.
Meza kuu wakiimba wimbo maarufu wa kabila la Kiha ‘ikidolidoli’.
Mgeni rasmi kwa kushirikiana na meza kuu wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa kwa vituo hivyo vya afya
Mkunga muuguzi wa kituo cha Afya Mwakizega, Mary Twakazi (kushoto) akitoa maelezo kuhusu kitanda maalum cha kujifungulia kinamama kilichotolewa na shirika la EngenderHealth.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na baadhi ya wafanyakazi wa mashirika wafadhili.
Toa Maoni Yako:
0 comments: