Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA)
wakiwa na baadhi ya vifaa kwa ajili ya kukabidhi Hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es
Salaam, ikiwa ni katika kuadhimisha Sikukuu ya Wanawake duniani.
Meneja Utawala na Utumishi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
(SSRA), Bi. Amina Ally, akikabidhi baadhi ya vifaa kwa Muuguzi Kiongozi wa wodi ya wazazi ya hospitali ya Mwananyamala, Sista Eva Njalla, Dar es Salaam katika kuadhimisha Sikukuu ya Wanawake duniani.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk. Daniel Nkungu (kushoto), akiwashukuru wafanyakazi wa SSRA, mara baada ya kupokea misaada hiyo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk. Daniel Nkungu (kulia), akiwatambulisha wafanyakazi wa SSRA kwa baadhi ya wafanyakazi wa hospitali hiyo.
Meneja Utawala na Utumishi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Amina Ally, akikabidhi baadhi ya msaada kwa mmoja wa wazazi waliokuwepo kwenye wodi hiyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: