Na Peter Sarungi (The Next Speaker)

Raisi wa Tanzania Mh. Magufuli alipo toa katazo la siasa za majukwaa na maandamano, wanasiasa hasa wa upinzani walikerwa sana na katazo hilo, ikapelekea upinzani kutangaza maandamano nchi nzima kupitia UKUTA ili kupinga katazo hili maana lili mruhusu Raisi pekee kufanya siasa hizo popote ndani ya Tanzania.

Kutokana na katazo hilo, tuliishauri Upinzani kubadili mikakati ili kutetea uwepo wa siasa zake. Mimi nilishauri kupitia andiko langu la "Ningekuwa mimi ni mbowe-part 1&2". Baada ya muda tulipata fununu za upinzani kuwekeza dolla za kutosha kwenye mitandao baada ya utafiti kuonyesha mapinduzi makubwa ya siasa katika mitandao kwa miaka ijayo. Hapo ndipo blogs na page mbalimbali nguli kama Tanzagiza zilipo shamiri kwa kutoa habari zenye mlengo wa kukosoa utawala na kupamba upinzani.

Leo tupo mwaka wa pili baada ya uchaguzi na bado miaka 3 tu ili uchaguzi mwingine ureje, mpaka sasa ni dhairi kwamba tumeanza kusahau zile siasa za majukwaa zilizokuwa na mbwembwe nyingi huku maudhurio yalikuwa na mashaka ya kukwaza dola, badala yake siasa zimehamia mtandaoni kwa nguvu nyingi huku faida ikimwangukia yule aliyewekeza rasilimali zake kwa wingi katika kupata wafuasi.

Wengi wetu tumesahau hata kuangalia, kusikiliza na kusoma habari kutoka vyombo vya habari tulivyo vizoea kama Radio, Tv na magazeti kutokana na uwepo wa habari hizo kupitia mitandao tena kwa wakati sahihi na wakati mwingine ni live badala ya kusubiri saa mbili usiku. Nguvu hii ya mitandao ndio ilimfanya Mkuu wa kaya kutamani kuzima mitandao kupitia malaika baada ya kuona hakuna kilicho badilika baada ya katazo lake la siasa mpaka 2020.

Nitumie makala hii kuwakumbusha wanachama na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama tawala CCM kutumia mikutano yake ya sasa na hata chaguzi za ndani zinazokuja kuweka agenda ya siasa za mitandao ili kuzitambua na hata kuwekeza vizuri kabla ya 2020. Nitashangaa sana kama swala la mitandao litaendelea kudharaulika bila kupewa kipaumbele eti kwa sababu ya kuenjoy holiday ya siasa za majukwaa kwa wapinzani na hata kubweteka na ruhusa aliyojipa mkuu wa kaya kwa siasa hizo za majukwaa. Bado hamjachelewa kumiliki siasa za mtandaoni ikiwa mtawekeza vya kutosha ili tucheze ngoma tofauti tofauti badala ya kila siku tunacheza ngoma za upinzani.

Nawatakia maandalizi mema ya mikutano yenu na chaguzi zenu zinazokuja.

Asanteni.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: