Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche akionesha kwa waandishi wa habari moja ya pombe kali aina ya kiroba original zilizokamatwa wakati wa operesheni inayoendelea mapema leo hii jijini Dar es Salaam wakati wa siku ya nne ya operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.
Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche akionesha kwa waandishi wa habari moja ya pombe kali aina ya kiroba original zilizokamatwa wakati wa operesheni inayoendelea mapema leo hii jijini Dar es Salaam wakati wa siku ya nne ya operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.
Afisa Afya toka Manispaa ya Kinondoni Bw. John Kijumbe (kilia) akichukua maelezo toka kwa mmiliki wa duka la kuuza vinywaji la Vunja Bei salasala Store Bw. Oscar Mujuni (katikati) wakati wa opereshe ya kusaka wauzaji wa pombe kali aina ya viroba ambayo Serikali imepiga marufuku matumizi yake, kushoto ni Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche.
Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche akifunga moja ya duka la jumla la vinywaji mara baada ya msimamizi wa duka hilo kuwakimbia maafisa wa Serikali wakati wa opereshe ya kusaka wauzaji wa pombe kali aina ya viroba ambayo Serikali imepiga marufuku matumizi yake mapema hii leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku ya nne ya operesheni hiyo.
Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche akionesha kwa waandishi wa habari moja ya pombe kali aina ya Nguvu zilizokamatwa wakati wa operesheni inayoendelea mapema leo hii jijini Dar es Salaam wakati wa siku ya nne ya operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.
Baadhi ya Maafisa wa Serikali wakiwa nje ya moja ya duka lililokutwa na pombe kali ambayo Serikali imepiga marufu kutumika mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa ghala la Love kira Enterprises lililopo Wazo Bi. Sia Mboya (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche (katikati) wakati wa operesheni ya kuondoa pombe hiyo katika soko, kulia ni Afisa Afya toka Manispaa ya Kinondoni Bw. John Kijumbe.
Gari lililokutwa limebeba pombe kali aina ya kiroba original likiwa limeegeshwa nje ya duka kuuza vinywaji la Love Kira lililopo Wazo jijini Dar es Salaam mapema hii leo.
Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo
Baadhi ya shehena ya pombe kali aina ya kiroba zilizokamatwa katika ghala la Kampuni ya Love Kira Enterprises lililopo Wazo jijini Dar es Salaam mapema hii leo.
Na: Lilian Lundo – MAELEZO.
Shehena ya pombe kali zilizofungwa katika vifungashio vya plastiki (Viroba) zenye thamani ya shilingi bilioni 2 zimekamatwa Jijini, Dar es Salaam katika operesheni inayoendelea ya kuondoa pombe hizo nchini.
Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Manchale Heche ameyasema hayo leo, Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na vyombo vya habari katika operesheni hiyo ambayo inaendelea kwa nchi nzima.
“Bado tunaendelea na operesheni ya ukamataji na uzuiaji wa pombe za viroba, ambapo leo katika ghala la kampuni ya Lovekira iliyoko Tegeta, Wazo tumefanikiwa kukamata zaidi ya katoni 7000 za pombe za viroba aina ya Konyagi, Valeur, Burudani na Zanzi ambazo ujazo wake ni kati ya mililita 50 mpaka 200,” alifafanua Heche.
Aliendelea kwa kusema kuwa, licha ya shehena ya viroba iliyokutwa katika ghala hilo bado kampuni hiyo inaendelea kuingiza mizigo ya viroba ambapo timu iliyofika kukagua ghala hilo ilikuta katoni nyingine za pombe hizo zikiwa ndani ya gari zikisubiri kuingizwa ndani ya ghala hilo.
Kwa upande wake Meneja wa kampuni hiyo Siah Mboya amesema kwamba, viroba vilivyokuwa ndani ya gari vilikuwa vikihamishwa kutoka tawi lingine la kampuni hiyo lililoko Tegeta kutokana na Serikali kusitisha uuzaji na usambazaji wa pombe hizo.
Aliendelea kwa kusema kuwa wamekuwa na shehena kubwa ya pombe hizo kutokana na kuwa na mzigo mkubwa ulionunuliwa kati ya mwaka 2014 hadi 2015. Aidha ameiomba Serikali kuongeza muda wa matumizi ya pombe hizo ili waweze kumaliza mzigo ambao bado upo katika maghala.
Nae, Afisa Afya wa Manispaa ya Kinondoni John Kijumbe amesema kwamba, baada ya kutambua idadi ya pombe za viroba iliyokamatwa. Muhusika wa mzigo uliokamatwa pamoja na Afisa wa Serikali husaini fomu inayotaja kiasi cha pombe kilichokamatwa na kupewa maelekezo ya kutoondoa mzigo huo mpaka Serikali itakapotoa maelekezo.
Operesheni ya kuondoa pombe za viroba ni utekelezaji wa tamko la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kusitisha uzalishaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya pombe hizo kuanzia Machi 01, 2017.
Aidha pombe hizo zimechangia kwa kiwango kikubwa uchafu wa mazingira, kupotea kwa nguvu kazi ya Taifa, ajali na vifo vilivyosababishwa na unywaji uliokithiri wa pombe hizo, kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu na kupotea kwa mapato yanayosababishwa na wafanyabiashara wasio waaminifu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: