Nakuomba Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohammed Shain, kwa heshima na taadhima naomba upokee salamu yangu ....Shikamoo Rais wa Zanzibar, pole na majukumu .

Pili naomba barua hii ya wazi ikufikie, Mh Rais barua hii nimeiandika ya wazi kwa sababu imebeba ujumbe wa raia wote wa Tanganyika.

Lengo la barua hii ni kuomba nchi yako ilipe deni la umeme ambayo serikali ya Tanganyika inakudai, Mh Rais sisi watanganyika tunanunua umeme wa Luku lakini bado tunakatiwa umeme.

Usiku tunalala giza mchana shuguli hazifanyiki ... ukiuliza sababu unaambiwa eti Serikali yako inadaiwa pesa nyingi na haujalipa, nakuomba ulipe umeme ili sisi watanganyika tupate nafuu. Kwa sababu Umeme si jambo la Muungano hivyo hatuwezi kusema kuwa umeme wetu niwa Tanzania bali niwaTanganyika.

Kama ungekuwa wa Muungano msingekuwa na shirika lenu la Umeme ambalo ni ZECO. Huku Tanganyika tukitumia Tanesco.

Naamini ombi langu litakufikia Mh Rais na utalifanyia kazi, kwani natambua umakini wako katika usimamizi wa serikali, umekuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya Zanzibar.

Hivyo naomba pia umakini wako uliouonyesha katika awamu ya pili ya utawala wa Benjamin William Mkapa na awamu ya kwanza wa Jakaya Kikwete ukifanya vizuri katika nafasi ya Makamu wa Rais pia uonyeshe umakini huo katika utawala wa Rais John Pombe Magufuli ili Tanzania tupate nchi ya viwanda.

Msaidie Rais Magufuli katika hili la kulipa deni la umeme ,natambua kuwa deni hilo umeliridhi kutoka kwa watangulizi wako ila huna jinzi naomba tu umsadie Rais wetu kwa kulipa deni la nchi yako ili tupate viwanda na tuachane na kero la katizo la umeme huku Tanganyika.

Wako katika ujenzi wa Tanzania ya viwanda.

JO ODOYO - HABARI MPYA.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: