Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Eliasi Tarimo akimkabidhi mmoja wa wasajili wa ndoa wa Manispaa ya Singida leseni ya usaajili wa ndoa. Hafla hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kituo cha Walimu cha Nyerere,mjini Singida.
Mmoja wa wasajili wa ndoa,Maalim Mayogho akimshukuru mkuu wa wilaya ya Singida kwa niaba ya wasajili 21 waliokabidhiwa leseni za ndoa kwenye hafla iliyohudhuriwa na waumini wasiopungua mia moja.
Baadhi ya wasajili wa ndoa wa wilaya ya Singida waliohudhuria hafla ya kupokea leseni za ndoa.
Mkuu wa wilaya ya Singida, Mhe. Elias Taraimo( wa pili kulia) wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi leseni za wasajili wa ndoa wa wilaya hiyo ili waweze kufanya shughuli hizo kwa kufuata sharia,kanuni na taratibu zilizowekwa.
Katibu wa Mkoa wa JASUTA,Bwana Yahaya Mohamedi (wa kwanza kutoka kulia) akisikiliza hotuba ya mkuu wa wilaya ya Singida( hayupo pichani),Bwana Eliasi Tarimo aliyotoa kwa wasajili wa ndoa wa wilaya ya Singida,kwenye hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kituo cha walimu cha Nyerere,mjini Singida.(Picha Na Jumbe Ismailly)
---
TAASISI isiyokuwa ya Kiserikali ya JAMAAT ANSWARU SUNNA TANZANIA (JASUTA) Mkoa wa Singida imepinga vikali Propoganda zinazoenezwa na baadhi ya watu wa ndani na nje ya nchi wa kukiuka utaratibu wa maumbile kwa kutaka kuhalalisha kuwepo kwa ndoa za jinsia moja nchini,na kuapa kwamba haitajihusisha na usajili wa ndoa za aina hiyo.
Hayo yamo katika risala ya Jumuiya hiyo iliyosomwa na Shabani Ramadhani Nkhomee kwenye hafla fupi ya kuwakabidhi leseni wasajili wa ndoa 21 wa JASUTA Mkoa wa Singida,hafla iliyofanyika kwenye kituo cha walimu Nyerere, mjini Singida.
“Nabii Luti (amani iwe juu yake ) watu wake waliangamizwa kwa kukiuka utaratibu wa maumbile Propoganda zilizopo za kuhalalisha ndoa za jinsia moja”alisema Nkhomee.
Aidha Nkhomee alisisitiza kuwa taasisi ya JASUTA inapinga vikali na kwa nguvu zote Propoganda zinazoenezwa na baadhi ya watu wa ndani na nje ya nchi wa kukiuka utaratibu wa maumbile kwa kutaka kuhalalisha kuwepo kwa ndoa za jinsia moja.
“Sisi tunapinga kwa nguvu zote Propoganda hizo na tunasema wazi kuwa hatutahusika kusajili ndoa hizo na tunaendelea kupinga hatua zote za kuhalalisha ndoa za jinsia moja kadri tuwezevyo”alisisitiza.
Akikabidhi leseni hizo kwa wasajili wa Taasisi hiyo,Mkuu wa wilaya ya Singida,Eliasi Tarimo aliweka wazi kwamba serikali haipo tayari kuunga mkono ndoa za jinsia moja.
Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya alibainisha kuwa kwa mujibu wa sheria na kwa mujibu wa mila za kitanzania,vitendo hivyo havina nafasi katika jamii ya Tanzani,kwani utaratibu huo ni mgeni kwa watanzania.
Kwa upande wake katibu wa JASUTA Mkoa wa Singida,Yahaya Mohamedi alisema katika siku za nyuma si kwamba wasajili hao walikuwa hawajishughulishi na shughuli za kuozesha na si kwamba ndoa walizokuwa wakizisimamia hazikusihi,hapana bali ndoa hizo zilisihi kabisa.
Lakini kaatibu huyo alifafanua kuwa kutokana na kuishi katika utaratibu wa kiutawala ni vema zaidi sote tukaingia katika utaratibu wa kiutawala utakaoirahisishia serikali katika kutekelza majukumu yake.
Hafla ya kuwakabidhi leseni wasajili 21 wa JASUTA Mkoa wa Singida,ilihudhuriwa pia na baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini na Taasisi zingine za dini ya Kiislamu zilizopo mjini Singida.
Toa Maoni Yako:
0 comments: