Meneja wa Jumo Tanzania, Rwebu Mutahaba akiongea na mawakala wa Airtel (hawapo pichani) wakati wa semina ya uzinduzi wa mpango utakaowawezesha mawakala wa Airtel Money katika mikoa mbalimbali kupata elimu ya huduma ya Airtel Timiza Wakala itakayowasaidia kupata mikopo isiyo na dhamana ili kukuza biashara zao . Semina ya mawakala iliyofanyika jijini Dar es saalam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya mawakala wa Airtel Money jijini Dar es Saalam wakifatilia kwa makini maelezo juu ya huduma ya Airtel Timiza yaliyotolewa kwenye semina ya mafunzo inayoshirikisha kampuni ya simu ya Airtel na washirika wake Jumo Tanzania
Meneja wa Jumo Tanzania, Rwebu Mutahaba akiongea na mawakala wa Airtel wakati wa semina ya uzinduzi wa mpango utakaowawezesha mawakala wa Airtel Money katika mikoa mbalimbali kupata elimu ya huduma ya Timiza itakayowasaidia kupata mikopo isiyo na dhamana ili kukuza biashara zao . Semina ya mawakala iliyofanyika jijini Dar es saalam mwishoni mwa wiki
Wakala wa Airtel Money wa maeneo ya msimbazi kariakoo bwana Maneno George akiuliza swali wakati wa semina ya uzinduzi wa mpango utakaowawezesha mawakala wa Airtel Money katika mikoa mbalimbali kupata elimu ya huduma ya Timiza itakayowasaidia kupata mikopo isiyo na dhamana ili kukuza biashara zao . Semina ya mawakala iliyofanyika jijini Dar es saalam mwishoni mwa wiki
---
Airtel Tanzania inatangaza uzinduzi wa mpango wake utakaowawezesha mawakala wa Airtel Money katika mikoa mbalimbali kupata elimu zaidi kuhusu fursa zinazopatikana katika bidhaa na huduma zake ikiwemo huduma ya Airtel Timiza wakala inayowawezesha mawakala kupata mikopo isiyo na masharti na kusaidia kukuza mitaji na biashara zao

Mafunzo hayo, ambayo yatawasilishwa kwa mawakala zaidi ya 1000 katika mikoa ya Dar es Salaam,Arusha, Mwanza Morogoro na Dodoma yameanza mwishoni mwa wiki katika mkoa wa Dar es salaam na yanategemea kumalizika agost 28 katika mkoani Morogoro .

Jackson Mmbando, Meneja wa Uhusiano wa Airtel Tanzania anasema, “Kusaidia biashara zistawi ni sehemu muhimu ya biashara ya Airtel na tuna shauku ya kuanzisha bidhaa za kibunifu zenye faida kwa jamii na wateja wetu wenye lengo la kuinua uchumi wao kote nchini. Mafanikio ya huduma ya mikopo ya Airtel Timiza yanatokana moja kwa moja na mtandao wetu mpana wa mawakala. tunaamini mafunzo haya yataongeza uelewa mkubwa zaidi wa huduma za kifedha zinazopatikana kwa mawakala wa Airtel Money.”

Timiza Wakala,ni huduma inayowawezesha mawakala wetu nchi nzima kupataa mtaji wa kufanyia kazi kupitia simu zao za mkononi,huduma hii iliyozinduliwa mwaka mmoja uliopita, kwa sasa mtandao wa mawakala 50,000 wa Airtel Money nchini Tanzania wanaweza kutumia huduma hii. Theluthi moja ya mawakala wote wa Airtel Money hutumia Timiza, na baadhi ya mawakala sasa hivi wanakidhi vigezo vya kupata mikopo hadi Shilingi milioni moja.

Akizungumzia kuhusu jinsi Mawakala wanavyonufaika na Timiza Wakala, Mmbando anasema “Utafiti wetu unaonyesha kwamba mawakala wengi hutumia Timiza wakala kuendesha biashara yao ya uwakala kwa kuweka pesa kwenye akaunti zao za Airtel Money kwaajili ya kufanya miamala na kuhudumia wateja. Wakala anaamua kiasi cha pesa wanachotaka kukopa pia na masharti ya marejesho, hivyo kuwapa udhibiti wa fedha zao”

Mmbando alisema Katika kipindi cha mwaka jana Timiza imekuaa kwa kiasi kikubwa na wateja wanathamini jinsi huduma hii inavyobadili maisha yao “Uhusiano kwa misingi ya kuaminiana umejengeka ambao unaturuhusu kutoa mikopo isiyo na dhamana kwa urahisi, wakati wowote mteja anapohitaji. Sambamba na hilo wateja wetu wanaelewa kwamba kuzingatia masharti ya mkopo ili kupata mikopo mikubwa na kutumia huduma ya Timiza kama benki”.

Tunayo mabadiliko tuliyoyafanya katika kuboresha huduma hii ya Timiza Wakala ikiwa nia pamoja na kuwapatia mawakala uwezo zaidi wa kuchagua jinsi ya kulipa mikopo mapema kwa mafungu na kupata mikopo mikubwa, lengo la semina za mafunzo haya ni kuwaelimisha mawakala ili kupata uelewa zaidi kulinganisha na ilivyo sasa. Huduma ya Airtel Timiza pia inawawezesha wateja wetu kupata mikopo isiyo ya dhamana ya hadi shillingi laki tano, mawakala na wateja nchi nzima kwa ujumla wanafaidia na huduma hii aliiongeza Mmbando

“Huduma ya Airtel Timiza imeendele kuungwa mkono na serikali na Benki kuu , na kuiwezesha Tanzania kuweka rekodi nzuri katika kuwapatia wananchi wake mazingira wezeshi yanayowanufaisha kifedha. Sisi Kama mtandao mkubwa zaidi wa simu nchini, tunajivunia mafanikio haya na kuendeleza dhamira yetu ya kutoa huduma za kibunifu za kifedha kwa wateja nchi nzima,” anahitimisha Mmbando.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: