Mwandishi Wetu

MWANDISHI wa habari Grace Khuni, amemuelekea Mungu kwa kuachia nyimbo tano za Injili ambazo zinatarajia kukamilika hivi karibuni.

Akizungumza hivi karibuni, Khuni alisema idadi kubwa ya nyimbo hizo zimekamilika ambako anaendelea kurekodi nyimbo hizo.

Khuni alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau kujipanga kupata neno la Mungu kupitia nyimbo hizo ambazo zina mguso ambao utasaidia jamii kumrudia Mungu.

“Nimeona kuna haja ya kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii ambayo inahitaji kukumbushwa kuhusu muumbaji wetu ambaye anatakiwa kuabudiwa muda wote,” alisema Khuni.

Aidha Khuni alizitaja nyimbo hizo ni pamoja na Vumilia, Wewe ni Mungu, Bwana anafanya njia, Kaa vizuri na Sifu jina la bwana.

“Naendelea na kuzifanyia kazi nyimbo nyingine ambazo zitakuwa moto wa kuotea mbali," alisema Khuni.

Khuni alisema anatarajia kuikamilisha albamu hiyo kabla ya Aprili ambako alitoa wito kwa wadau mbalimbali wa muziki wa Injili kuipokea kazi yake.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: