Kama kuna jambo limefichwa usoni pa wanadamu ni KIFO. Tungelijua sijui tungekuwa na aina gani ya Maisha...

Labda tusingesoma, labda tusingejenga nyumba, labda tusingeoa na kuolewa, labda tusingezaa watoto na yamkini tusingenunua magari wala kusafiri kwa kutumia magari hayo... inabaki kuwa fumbo!
 Leo imekuwa siku ngumu na mbaya ambayo itabaki kuwa kovu kwa maisha yote kwa Rev.Dr Pastory Michael Majembe ambaye ni mchungaji wa TAG - Ebenezer (Dodoma) Mwanataaluma mahiri wa Theolojia, na Mwalimu wa Chuo biblia Dodoma (Central Bible College, zamani AGBC) na familia yake, Kanisa la TAG kwa ujumla, ndugu jamaa na marafiki... baada ya kupata Ajali ya Gari akiwa na familia yake, juzi (jumatano) katikati ya Mtera na Mpunguzi, Mkoani Dodoma na Kupoteza Watoto wake Wanne kwa pamoja Junior, Isack, Gabriel na Glady katika ajali hiyo.
Mchungaji Pastory Majembe na Mama Bwana amewaponya, bado wanahitaji maombi maana nao wamepatwa na Majeraha na wanaendelea na matibabu...

Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: