
Waandishi wa habari wakiongozwa na Meneja wa Kiwanda cha kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond(wa kwanza kushoto), kwenda kutembelea mtambo unaotumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba kuzalisha nishati ya umeme inyotumika kuendesha mitambo ya kiwanda hicho.Kulia ni Meneja wa Maji na Nishati wa TBL, Sunday Kidolezi.
Meneja wa Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,Raymond Richmond (mwenye shati jeupe) akiwaonesha waandishi wa habari mtambo unaozalisha nishati ya umeme kwa kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba kwa ajili ya kuendesha mitambo ya kiwanda hicho.anaoshuhudia ni Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo,Sunday Kidolezi (mwenye fulana ya mistari).Mwingine ni mwandishi wa habari wa kampuni ya The Guardian, Daniel Mkate,ambaye ni miongoni mwa waandishi wa habari waliotembelea kiwanda hicho.
Mwandishi wa habari, Daniel Mkate (kushoto) akiwauliza maswali, Meneja wa Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond na Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo, Sunday Kidolezi, kuhusu changamoto ya upatikanaji wa mali ghafi hiyo na madhara yake katika kuzalisha nishati na athari za mazingira.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Kampuni ya Bi (TBL) Mwanza,wakijaza mapumba kwenye magunia, kabla ya kuingizwa kwenye mtambo wa kuzalisha umeme kiwandani hapo.Hapo ni katika eneo linalotumika kupakulia shehena ya mapumba hayo ya mchele, kutoka kwa msambazaji.
Meneja wa kiwanda cha Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,Raymond Richmod, akiwaonyesha waandishi wa habari, Daniel Mkate wa TRhe Guardian (nyuma) na Henry Kavirondo wa Chanel Ten,mashine inayosukuma mapumba ya mchele na mashudu ya pamba, kwenda kwenye mtambo wa kufua umeme unaotumika kuendesha mitambo ya kiwanda hicho.Kulia ni Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo, Sunday Kidolezi.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,wakijaza mapumba ya mchele kwenye mashine kwa ajili ya kuyasukuma kadi kwenye mtambo wa kuzalisha nishati ya umeme, unaotumiwa kuendesha mitambo ya uzalishaji ya kiwanda hicho.
Meneja wa Maji na Nishati wa kiwanda cha Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Sunday Kidolezi, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhudu mradi huo wa uzalishaji wa nishati ya umeme,unaotumika kuendesha mitambo ya kiwanda cha kampuni hiyo kwa kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba.Wa kwanza kushoto ni Meneja wa kiwanda cha kampuni hiyo,Raymond Richmond.
Toa Maoni Yako:
0 comments: