Shukrani za pekee zimfikie Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Peter Pinda, Mawaziri, Wabunge, Wakuuwa Mashirikana Wafanyakazi wa Serikali kwa kutufariji kipindi chote cha kuumwa kwake mpaka alipotwaliwa kutoka ulimwengu huu.
Shukrani za pekee pia ziwafikie wafanyakazi na wajumbe wa bodi ya NHC, Serengeti Breweries, DAWASCO, KCB, Rafiki Club, Soul Sisters, New Millenium Women Group, Beach Ladies, Sisters Club, Madaktari na wauguzi wa hospitali za Muhimbili, Hindu Mandal, Apollo Hydrabadna Dispensary yaArafa.
Mapadri na wachungaji wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Mbezi Beach, Makanisa ya Anglikana ya Mtakatifu Paulo la Ukonga, Dar es Salaam na Mtakatifu Petro la Mkuzi,Tanga, kwaya mbalimbali na vikundi vya maombi kwa msaada wao wa kiroho.
Tunawakushukuru mtu mmoja mmoja lakini haiwezekani kwani watu ni wengi sana, tunaomba tu mpokee shukrani zetu za dhati kutoka moyoni mwetu kwajinsi mlivyotufariji katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa baba yetu.
Misa ya Shukrani
Familia ya marehemu Dr. John Edward Mchechu wanapenda kuwakaribisha wote katika misa ya shukrani itakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 12/09/2015 kuanzia saa mbili asubuhi katika kanisa la Mtakatifu Petro Mkuzi, Tanga. Karibuni sana mjumuike nasi.
Raha ya milele umpeeeh Bwana wamilele umwangazie apumzike kwa amani, Amina
MR. & MRS. NEHEMIAH MCHECHU.
Toa Maoni Yako:
0 comments: