Vikosi mbali mbali ya Majeshi vikiwa vimejipanga tayari kwa kungia uwanjani kwa ajili ya ufunguzi wa michezo ya majeshi 2015.
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni mkuu wa Wilaya ya Songea Prof. Nomarn Sigalla King akisalimiana na wachezaji wa timu ya jeshi kutoka Mtwara.
---
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Prof. Norman Sigalla King akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya The Might Elephant .
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Prof. Norman Sigalla King akionyesha ufundi wake wa kumiliki mpira katika ufunguzi wa michezo ya majeshi.

Na Amon Mtega ,SONGEA

MICHEZO ya majeshi inayoshirikisha vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama briged ya kanda 
ya kusini imefunguliwa rasmi na kaimu mkuu wa mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Songea ,Pr Noman sigaa King huku benki ya NMB tawi la Songea likiwa limetoa msaada wa jezi za mpira wa miguu seti saba ambazo zenye thamani ya shilingi 3,000,000.

Akiongea kwenye ufunguzi huo uliyofanyika leo katika uwanja wa michezo wa majimaji uliyopo Songea ,Sigara alisema kuwa michezo hiyo itaimarisha mahusiano ya kiulinzi baina ya mipaka yetu ya Tanzania kwa kuwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama vitakuwa na ushirikiano.

Alisema kuwa ulinzi wa Tanzania katika mipaka yetu  hautegemei jeshi moja tuu bali ni ushirikiano wa vikosi vya majeshi mbalimbali kama vikosi hivi ambavyo vimeshirikishwa kwenye michezo hii
iliyozinduliwa na ambayo itarajiwa kufanyika kwa wiki mbili.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: