Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama  Shekha Nasser Katikati  akiongea na Vyombo vya Habari leo wakati akelezea Mandalizi ya Uzinduzi wa Manjano Foundation Ambao ni Mpango unaolenga kuwawezesha Kutoa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa Wasichana wa Kitanzania.Mpango Uzinduzi huu utafanyika tarehe 31 Mei 2015 kuanzia saa 6 mchana kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee VIP Hall. Utatoa fursa kwa kuendeleza mtandao wa kibiashara kwa kina mama na pia mada mbali mbali ya jinsi ya kujikwamua kimaisha itatolewa. Bila ya kusahau mafunzo ya jinsi ya kutumia vipodozi. Mgeni Rasmi anategemewa Kuwa Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda
 Meneja Mradi wa Manjano Foundation Mama Gugu Ndolvu Akieleza jambo leo wakati wakiongea na wanahabari kuhusu Mradi huo ambao ni Mkombozi kwa wakinamama wasio na Ajira Akiwa samabamba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama  Shekha Nasser  Pamoja na  Aunty Sadaka Gandi
 Aunty Sadaka Gandi akiwa ni dada mkuu wa Atakayewashauri wasichana watakaopata mafunzo ya ujasiriamali kupitia Manjano Foundation. 
Wasichana waliochaguliwa kunufaika na Mpango hup wakiwa Katika Picha ya Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama  Shekha Nasser  

Shear Illusions inasherehekea mwongo mmoja wa urembo nchini Tanzania kwa kuzindua 
vipodozi vyake ijulikanayo kama LuvTouch Manjano! 

Uzinduzi huu utafanyika tarehe 31 Mei 2015 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee VIP Hall. Shamrashamra hizi pia itatoa fursa kwa kuendeleza mtandao wa kibiashara kwa kina mama na pia mada mbali mbali ya jinsi ya kujikwamua kimaisha itatolewa. Bila ya kusahau mafunzo ya jinsi ya kutumia vipodozi.

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda na mtoa mada mkuu atakuwa ni Balozi Mwanaidi Majaar.

Shear Illusions, imeweza kutambulisha urembo na muonekano wa mwanamke wa kitanzania 
kwa Zaidi ya miaka kumi. Wamebaisha urembo kuanzia kujipodoa, nywele, vipodozi 
na vito hadi blog na jarida inayoelezea masuala ya urembo. Baada ya kuuza bidhaa mbali mbali ya urembo toka nchi mbali mbali, Shear Illusions inazindua rasmi bidhaa yake ya LuvTouch Manjano.

LuvTouch Manjano ni maalum kwa ajili ya kumpendezesha mwanamke wa kitanzania. Kuna aina 
kumi ya vipodozi msingi kuanzia Mwanzi na Mpodo hadi kahawa na ardhi. Bidhaa hizi zimezingatia hali ya hewa ya joto. Vipodozi hivi vinalengo la kuongeza muonekano wako kwa hali yoyote.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: