Nilistuka nikamuuliza unawaza nini akasema hakuna kitu, anashagaa tu, basi nikamwambia usihofu nikajaribu utundu wangu wote ila wala hata gari halikuwaka, ikabidi aniambie nimuache tukaenda kulala... wakati nimeamka majira ya saa 8 usiku niende chooni nashangaa mume wangu hayupo kitandani, niliogopa sana nikabidi nianze kukagua kaenda wapi??? nilianza kupitia chooni nikamkosa, kuandalia sebule ya juu hayupo, nikaenda kwenye upenyo nikachungulia sebule ya chini namuona amekaa anaangalia movie, amevaa taulo tu.
Nikashuka hadi chini, nikamuuliza unashida gani usiku huu??? watu wamelala wewe unaangali movie, akasema niache sina usingizi, kuangalia pembeni yuko na simu yangu... moyo ukafanya pwaa!!!
Nikamuuliza mbona umekaa na simu yangu, akasema SINA MIPAKA JUU YA SIMU YAKO MKE WANGU... nikataka kuichukuwa kwa nguvu, akanikalipia akasema nisipende kutumia nguvu sana nitaumia... akanipa simu yangu na akaniambia nikalale, wakati huo yeye alikuwa pale anaangalia movie huku anakunywa wine.
Alikuwa anaangalia CD moja ambayo nilitamani kila mtu angekuwa nayo inaitwa FIND A SECRET... nzuri sana... nikamuuliza uliichukua ya nini simu yangu???, akasemea nilipize basi nenda nayo na yangu.
Sikumjibu nikarudi zangu kwenda kulala, wakati nimefika kitandani nikaanza kupekua meseji, sikukuta mesaji hata moja, nikajipa moyo sikujua kumbe Kelvin alikuwa alirudisha majibu, alinisifia tulipofanya mapenzi, nikahisi mme wangu akajifowadia ile mesaji maana siku ananiacha kanisani aliionyesha na akasema anazo meseji zote kwa vile alienda mtandao wa simu niliokuwa natumia akapatiwa tulikuwa tunatumiana, basi nilipojiridhisha tu nikalala usingizi hauji nikaseam au katuona?
Nilipitiwa na usingizi nikalala, hali ilianza kubadirika hapo, simuelewi kabisa mwenzangu, anauchuna tu, haniulizi chochote ni kama ndani ya miezi sita niko na Kelvin mambo moto moto... kuna siku akanaimbia mke wangu nataka kukutoa nikamuuliza wapi? Akasema nahitaji kuongea na mimi omba ruhusa kazini WAAMBIE UNAUMWA TENA... nahitaji kwenda na wewe Zanzibar.
Mh mh! nikastuka hiyo tena imetoka wapi? Nikamuuliza niwaambie tena kwani nishawahi kuomba ruhusa ya kuumwa, akasema aah! nilikosea kuongea tu, don’t mind, we omba ruhusa.
Niliomba tukaenda hadi Zanzibar tukafikia hotelini, lakini safari ile ilikuwa ni kuongea tu... ananisihi nitulie, kama kuna shida niseme, kama kuna tatizo tuongee ananipenda sana... yani aliongea kupita kiasi, nikasema kwani kuna nini???, najikausha akasema ah! moyo tu hauna amani, tukafurahia kidogo akaninunulia madraya ya mkono ya kutumia mwenyewe nisiende salon, yani alinifanyia kila kitu hao tukarudi Dar.
Kufika tu ugomvi ukaanza na Kelvin kwa simu, anasema kwanini niliondoka bila nikamwambia nilikuwa na mme wangu, na ilikuwa ghafla, na nilikuwa nimebanwa nisingeweza kabisa kuongea na simu, akachukia akaanza utuma meseji za ajabu ajabu.
Tukiwa tumekaa sebuleni niko busy na simu yangu, sina hili wala lile, Franco akasema mke wangu SIKU NIKIGUNDUA UNANIDANGANYA, NITAKACHOKUFANYA KITU AMBACHO HAUTASAHAU MAISHANI KWAKO... nikamwambia kwani nini, basi nikazuga hapo kimoyo moyo nikasema nitakuwa makini zaidi.
Tulikaa kama miezi miwili amani ikiwepo kabisa nyumbani kwangu, japo sio sana, tukawa tumepanga twende kwa mama yangu, tukamsalimie yuko Kigoma, tukaenda na mme wangu hadi Kigoma nashangaa nimefika nae Kelvin ananipigia simu nae yuko Kigoma eti alinifanya nikasema siwezi kukuona akasema haiwezekani, lazima tuonane, basi nikadanganya kuwa naenda kwa dada yangu mkubwa, mume wangu aniruhusu niende tu, akasema mie nimekuja kwenu... wewe ndiyo mwenyeji wangu, unaniacha na huyu mama naongea nae nini?
Kuna mipaka mimi kwenda kwa ndugu zako hadi uende peke yako??? Nikasema hakuna, nilichokaa maana nilikuwa nimemuelekeza Kelvin aje maeneo hayo, na mimi huku mume wangu akaniambia twende wote ikabidi nimwambie Kelvin asije.
Sijui hadi leo, mme wangu aliisomaje ile meseji maana nilikuwa nikituma tu naifuta, wakati tunarudi jijini Dar akaniuliza vipi, mbona ulimzuia mwenzio, kuja kwa dada yako, nikasema nani? Akasema ah!!! ACHANA NAYO HAYO, NIKASEMA NAMBA, NIAMBIE UNAMAANISHA NINI? AKASEMA yaache tuendelee na mengine... akaanza kuongea mengine, nilistuka kidogo ila mwenzangu akawa sawa tu, tulipofika Dar, ugomvi ukaanza na Kelvin kwanini nilimzimia simu, ugomvi mkubwa sana... nikaaendelea kuchelewa nyumbani.
Endelea kufuatilia sehemu ya nne... itawajia kesho....
Mmmh jamani kwa kweli ni ngumu
ReplyDeleteMmhh !!!
ReplyDeleteMmhh !!!
ReplyDeleteDah!
ReplyDelete