Nilizaliwa kwenye familia ya watoto sita nikiwa mtoto pekee mwenye albinism. Mama alitupenda na anatupenda sawa bila kujali hali yangu na kunifanya nijione sawa na wenzangu. Tunapendana sana. (Pichani ni Bi. Clara Peter akiwa na mwanae).
Nilizaliwa kwenye familia ya watoto sita nikiwa mtoto pekee mwenye albinism. Mama alitupenda na anatupenda sawa bila kujali hali yangu na kunifanya nijione sawa na wenzangu. Tunapendana sana. 

Hali hii ilinifanya nisijute na wala haitokaa itokee nijute kuzaliwa na hali (mwenye albinism). Mungu aliniumba kwa kusudi lake, kusudi maalum na wala si kwa bahati mbaya. Ila kusudi hili linaharibiwa na kukatishwa na baadhi ya wapumbavu (wauaji) wenye fikra mgando. Ila bado sijakata tamaa nitapambana mpaka dakika za mwisho za pumzi yangu.

Moyo wangu unavuja damu, damu na maji, japo bado nina tumaini la kuishi, moyo wangu huu umekunja ngumi ambayo sijui itatua kwa nani kwani adui yangu simjui. Je Ni familia, wazazi na ndugu zangu, majirani na marafiki au watu kuja nisowajua?

Hivi ni nani hasa anayedhamini mauaji haya ya kikatitili kwa watu waenye albinisim? Hakika hii ni system pana tena pana sana yenye kujitosheleza katika kila Nyanja. System inayolindwa kama nyara za serikali ama hata zaidi ya nyara hizo, kwani siamini kama serikali yetu hii ya maisha bora kwa kila mtanzania imeshindwa kuwakamata wahusika. 

Muda mwingine najiuliza hivi mauaji haya yanasababishwa na imani za kishirikina tu au kuna mengine chini ya mwamvuli huu mpana wa imani za kishirikina? Mh! Mimi na wewe hatujui. Na je soko kuu la bidhaa hizi haramu lipo wapi na nani ana hisa nyingi? Pia mimi na wewe hatujui. Kuna connection gani kati ya hawa majasusi wauaji na watunza usalama? Mbona inakuwa ngumu kuwatia mikononi mwa sheria? ama kwa hakika kuna jambo zito ambalo limejificha chini ya kapeti ambalo mimi na wewe hatuljui.

Naamini kwa kutumia teknolojia ya sasa na hasa ya mawasiliano kuyakamata haya majitu mauji kuanzia jani, tawi, shina na hata mzizi wake, mwezi ni mrefu.

Mtukufu Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete watu wenye albinism tunakulilia baba tunaomba utuokoe sisi wana wa Israel tunapukukutika kwani tunaamini AMRI yako itasaidia kusitisha tatizo hili ikiwemo ya kunyongwa mpaka kufa kwa wote waliobainika kuhusika na uchafu huu. 

Tunaomba haki itendeke kwa familia zilizopoteza wapendwa wao na wahanga wote. Tunahitaji uhuru katika nchi yetu, tunahitaji amani na upendo. Mbona tuishi kwa kujifichaficha kama wahalifu wa mihadarati katika nchi yetu? Hatuna hatia wala hatuna bahati yoyote badala yake tumekosa vimelea vinavyosababisha rangi ya asili (melanin) MSITUUE hakuna tulichotofautiana. 

WE NEED NO WE DIMAND JUSTICE
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: