Katibu wa Nchi kutoka Wizara inayohusika na Masuala ya Uchumi na Nishati ya Ujerumani, Mattias Machnig, akiangalia zawadi aliyopewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Monica Mwamunyange, wakati Katibu huyo na ujumbe wa wafanyabishara kutoka nchini Ujerumani walipotembelea wizarani hapo leo asubuhi ili kujifunza fursa za uwekezaji katika sekta Uchukuzi.
Katibu wa Nchi kutoka Wizara inayohusika na Masuala ya Uchumi na Nishati ya Ujerumani, Mattias Machnig, akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, leo Wizarani mara baada ya Katibu huyo na ujumbe wa wafanyabishara kuembelea wizara hiyo. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania(TRL), Mhandisi Kipalo Kisamfu.
Mkuu wa Idara ya Sera za kilimo na Maswala ya Biashara katika Wizara inayohusika na Masuala ya Uchumi na Nishati ya Ujerumani, Monica Ottemeyer akifurahia jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Monica Mwamunyange mara baada ya Ujumbe huo kutoka Ujerumani kutembelea Wizara hiyo Leo Asubuhi, ili kujua miradi mbalimbali ambayo Serikali ya Ujerumani inayoweza kuweekeza ili kuinua uchumi wa Tanzania.

Picha na Kitengo Cha Mawasilino Serikali-Uchukuzi)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: