Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imezuia maandamano ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya Ilala (UVCCM) ya kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa chama hicho pamoja na kuacha kiporo  maandamano ya Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha).

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ,Kamishina wa Jeshi la Polisi ,Suleiman Kova ,amesema kuzuia kwa maandamano hayo inatokana na kuwepo kwa taarifa za Kiintelejensia za kuvuruga amani.

Kova amesema maandamano ya UVCCM Wilaya ya Ilala yalitakiwa kufanyika kesho lakini kutokana na kuwepo kwa taarifa za kiintelejensia za Machinga ,Bodaboda ,Mama Lishe na Baba Lishe kushiriki maandamano na kufikisha malalamiko yao kupitia maandamano hayo.

Amesema kumekuwepo kwa taarifa katika mitandao ya jamii wakihamasishana bodaboda na machinga ,mama lishe na baba lishe kushiriki maandamano pamoja na kutoa ujumbe wao kwa kupitia maandamano katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Kova amesema machinga, Mama lishe, Baba, na Bodaboda watumie taratibu zingine za kufikisha ujumbe kutokana na sheria zilizowekwa na sio kutumia mgongo katika vyama vya siasa.

Kwa upande Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) maandamano yao yalikuwa yanahusu kwenda tume ya Taifa ya Uchaguzi ni lini itaanza kuandikisha daftari la wapiga kura, pamoja na wanafunzi watashiriki vipi upigaji kura ambapo Kamanda Kova amesema hilo wanaweka kiporo kwanza wanafanya uchunguzi wa taarifa mbalimbali.

“Sisi tunachoangalia amani kwani maandamano ya amani yanaweza kufanyika lakini mwisho wa siku inakuwa sio amani kwa jeshi la polisi tunawajibu kuangalia hilo”amesema Kamanda Kova.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: