Meneja Usambazaji na Matawi, Bi. Masala Korosso wa FNB Tanzania akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa matawi mapya ya benki hiyo yaliyofunguliwa Sinza Kijiweni na Mbagala Zakhem kwa lengo kusogeza huduma kwa wateja pamoja na kuhudumia biashara ndogo na za kati zinazokua kwa kasi katika maeneo hayo. Kushoto ni Meneja Huduma za Rejareja wa Benki hiyo Emmanuel Mongella (Picha: Executive Solutions).
Meneja Huduma za Rejareja wa FNB Tanzania Emmanuel Mongella Meneja Usambazaji akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa matawi mapya ya benki hiyo yaliyofunguliwa Sinza Kijiweni na Mbagala Zakhem kwa lengo kusogeza huduma kwa wateja pamoja na kuhudumia biashara ndogo na za kati zinazokua kwa kasi katika maeneo hayo. Kushoto ni Meneja Matawi, Bi. Masala Korosso (Picha: Executive Solutions.
Na Mwandishi Wetu.
First National Bank imeongeza huduma zake kwa maeneo mengi zaidi ya jiji la Dar es salaam kwa kufungua matawi mawili mapya katika maeneo ya Sinza na Mbagala. Hii inaifanya benki hiyo kuwa na jumla ya matawi saba yaliyofunguliwa katika kipindi cha miaka mitatu.
Meneja wa Huduma za Rejareja wa First National Bank, Emmanuel Mongella amesema kuwa matawi mapya yatakidhi mahitaji ya huduma za kibenki kutoka benki hiyo ambayo yanaendelea kuongezeka na matawi haya yatahudumia wateja wa reja reja na wateja wa biashara katika maeneo haya ambayo yana biashara ndogo na za kati zinazokua kwa kasi sana. Matawi haya yanakuja na huduma zilizolenga kukidhi mahitaji mbalimbali ya wateja na jumuiya za biashara katika maeneo hayo.
"Tuna imani kuwa matawi haya yatafanikiwa na tuna mipango kabambe ya kufungua matawi kwenye maeneo mengine tukianza na Arusha na Mwanza kabla ya mwisho wa mwaka huu,” alisema Mongella.
Meneja Usambazaji na Matawi, Masala Korosso alisistiza kwamba benki imechagua kuwekeza katika maeneo haya kutokana na ukuaji kasi wa jiji la Dar es salaam na kuongeza kuwa tawi la Sinza liko eneo la Kijiweni na tawi la Mbagala liko eneo la Rangi Tatu.
Alisema kuwa Sinza na Mbagala ni maeneo muhimu kuwekeza na ndio maana FNB imeona ni wakati muafaka kuanzisha huduma zake kwenye maeneo hayo. “Kwa pamoja Sinza na Mbagala ni maeneo ambayo yanakua sana kiuchumi na hii imetulazimu kuhakikisha uwepo wa FNB katika maeneo haya”.
Ufunguzi wa matawi haya utaongeza huduma ambayo tayari inatolewa na FNB kupiti tawi la Kariakoo lililoko mtaa wa Uhuru, tawi la Makao Makuu eneo la Posta, tawi la Viwandani lililopo Quality Centre, Peninsula lililopo Oysterbay na Kimweri lililopo Msasani.
FNB ni benki iliyosambaa barani Afrika iliyoanza kutoa huduma kusini mwa jangwa la Sahara tangu mwaka 1874. Hivi sasa FNB inapatikana Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Zambia, Mozambique, Lesotho, Swaziland na Tanzania. Benki hii imedhamiria kuwa taasisi bora zaidi ya kifedha barani Afrika.
FNB Tanzania ilifungua milango yake rasmi nchini Tanzania mnamo Julai 27, 2011. FNB ina dhumuni kubwa la kuwa mdau muhimu katika maendeleo ya sekta ya fedha na imejipanga kuendelea kuanzisha huduma zenye ubunifu na utaalamu wa hali ya juu hapa nchini.
Ubora wa huduma na ufunguaji akaunti haraka pamoja na utoaji wa kadi za ATM za Visa ndio zinaitofautisha FNB katika soko na hakika FNB inazingatia kauli mbiu yake isemayo “Tukusaidieje?”
Toa Maoni Yako:
0 comments: