Vijana wa Chama cha Watafuta Njia (PF), kutoka kanisa la Waadiventista Wasabato Kigamboni, wakimvalisha Skafu Mwenyekti wa Konference ya Kusini Mwa Tanzania, Mchungaji Mark Marekana (wa pili kutoka kulia), kabla ya kuweka jiwe la msingi katika kanisa la waadventista wasabato Kigamboni,jana mchana.
Katibu Mkuu wa Unioni ya Kaskazini mwa Tanzania, Mchungaji Davis Fue, akiangalia ramani ya jengo la kanisa la Waadventista Wasabato litakavyokuwa mara baada ya kumalizika, wakati wa uwekaji jiwe la msingi la kanisa hilo jana mchana, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Extra Vaganza, ambayo yanafanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwaya ya Kanisa la Waadventista Wasabato Kigamboni, wakiimba kabla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kanisa la Waadventista Wasabato Kigamboni. Jiwe hilo la msingi liliwekwa jana na Katibu Mkuu wa Divisheni ya Afrika Mashariki na kati wa Kanisa la Waadiventista Wasabato, Dkt. Nathaniel Walemba kwa niaba ya Mwenyekiti wa Divisheni ya Afrika Mashariki na kati wa Kanisa la Waadiventista Wasabato, Mchungaji, Dkt. Blasious Ruguri.
Katibu Mkuu wa Divisheni ya Afrika Mashariki na kati wa Kanisa la Waadiventista Wasabato, Dkt. Nathaniel Walemba, akifungua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la kanisa la Waadiventista Wasabato Kigamboni jana mchana, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya extra vaganza yanayoendelea katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Divisheni ya Afrika Mashariki na kati wa Kanisa la Waadiventista Wasabato, Dkt. Nathaniel Walemba, (wa nne kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Kanisa la Wasabato kigamboni, wazee wa kanisa hilo na baadhi ya washiriki wa kanisa hilo, jana mchana mara baada ya kuweka jiwe la msingi. Wa nne kutoka kulia ni Katibu wa Union ya Kusini Mwa Tanzania, Mchungaji James Machage.
Picha na Lisso Ibrahim Biseko
Toa Maoni Yako:
0 comments: