Serikali ya wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFMSO), kupitia msemaji wake mkuu ambaye ni Rais wa Serikali ya wanafunzi, ndugu Clinton Boniface inakanusha taarifa zilizotolewa na gazeti la NIPASHE toleo namba 0578395 la tarehe 19/02/2015, lenye kichwa cha habari “WANAFUNZI WA IFM WAMTAKA LOWASA URAIS” na kwamba habari hizo hazijatolewa na uongozi wa IFMSO, wala hakuna mkutano wowote uliofanyika katika eneo la chuo cha usimamizi wa fedha kati ya waandishi wa habari na uongozi wa serikali ya wanafunzi na kutoa tamko hilo. 

Pia, kulingana na Katiba ya IFMSO kifungu namba 3, ibara ndogo ya 1, Katiba inakataza serikali ya wanafunzi (IFMSO) kushiriki katika mambo yoyote ya kidini au kisiasa, hivyo basi IFMSO inasikitishwa na taarifa hizo na inaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kutokana na taarifa hizo.

Imetolewa na;
------------------
Clinton Boniface.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi.
IFM-SO
19/ 02/ 2015.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: