Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Richard Martin almaarufu kwa jina la Rich Mavoko amesaidi mkataba mnono wa kuwa balozi kwenye Shirika la WWF (World Wide Fund). 

Akizungumza na Kajunason Blog, Msanii Rich Mavoko alisema anamshukuru Mungu kwa kuweza kumsimamia na kumfungulia milango ya kuwa balozi wa shirika hilo.

Kazi ya Msanii Rich Mavoko ni kusimamia mradi uitwao 'Solar for Education' ambapo mradi huo unakazi ya kusambaza na kuhakikisha shule za vijijini zinatumia umeme wa nishati ya jua.

Shirika hili limewahi kufanya kazi na watu maarufu mbalimbali duniani kama mabalozi kwenye kazi zao mbalimbali. 

WWF ni shirika lisilo la kibiashara lenye makao makuu nchini Switzerland. Shirika hili hupata fedha kutoka World Bank, serikalini, watu binafsi na makampuni ya kibiashara.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: