Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh. Khamisi Haji Khamis akiongoza Sala ya kuusalia mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin, katika masjid Muhammad Mombasa kwa Mchina, katika Sala hiyo amehudhuria Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk. Amani Karume, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, na Viongozi mbalimbali wa Vyama vya Siasa Tanzania.
Waumini wa Dini ya Kiislam wakiusalia mwili wa Marehemu Salmin Awadh Salmin, katika Masjdi Muhammed Mombasa kwa Mchina.
Shekh Othman Maalim akisoma dua baada ya kuusalia mwili wa marehemu Salmi Awadh, katika Masjid Muhammed Mombasa kwa Mchina na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali na Wananchi wa Zanzibar na Nje ya Zanzibar.
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiitikia dua baada ya kuusalia mwili wa marehemu katika Masjid Muhammad Mombasa kwa Mchina
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal. akisalimiana na Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume baada ya kusalima maiti katika Masjid Muhammad mombasa.
Wananchi wa Zanzibar wakishiriki katika Mazishi ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mhe. Salmin Awadh Salmin yaliofanyika katika Masjid Muhammad Mombasa kwa Mchina
Asakari wa Baraza la Wawakilishi wakibeba jeneza lililokuwa na Mwili wa Marehemu Salmin Awadh Salmin wakiwa katika Kijiji cha Kijini Makunduchi Wilaya ya Kusinu Unguja tayari kwa mazishi hayo.
Wananchi wakiwa makaburimi katika mazishi ya Mwakilishi wa Magomeni Zanzibar katika Kijiji cha Kijini Makunduchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiongoza mazishi ya mwakilishi wa magomeni yaliofanyika katika Kijiji cha Kijini Makunduchi Unguja Wilaya ya Kusini Unguja,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akishiriki katika mazishi ya marehemu Salmin Awadh Salmin, aliyekuwa Mwakilishi ya Jimbo la Magomeni na Mnadhimu wa CCM katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar, akiweka mchanga kaburini.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Saimin Awadh Salmin wakati wa maziko yake yaliofanyika Kijini Makunduchi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiweka mchanga katika kaburi baada ya kuzikwa mwili wa Marehemu Salmin Awadh Salmin katika kijiji cha kijini makunduchi.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg. Vuai Ali Vuai, akiweka mchanga kaburini.wakati wa maziko ya mwakilishi wa magomeni Zanzibar.
Waziri Mkuu Mstaaf wa Tanzania Mhe Edward Lowasa akishiriki katika mazishi ya mwakilishi wa magombeni yaliofanyika kijiji kwao kijini makunduchi Zanzibar, akiweka mchanga katika kaburi.
Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum Mark Mwandosa akishiriki katika mzishi hayo akiweka mchanga kaburini wakati wa mazishi hayo yaliofanyika katika Kijiji cha Kijini Makunduchi Zanzibar.
Shekh Hassan Kanji akisoma dua ya kumsomaa maiti wakati wa mazishi yaliofanyika katika makaburi ya Kijini Makunduchi Zanzibar.
Waheshimiwa Viongozi wakiitikia dua baada ya aziko ya mwakilishi wa magombeni yaliofanyika Kijiji kwao Kijini Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.
Waheshimiwa wakishiriki katika kuitikia dua.
Wananchi wakishiriki katikac dua ya kumuombea marehemu.
Wananchi wakishiriki katikac dua ya kumuombea marehemu.
Na Rajab Mkasaba, Ikulu - Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein leo ameongoza mazishi ya marehemu Salmin Awadh Salmin aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Zanzibar tangu mwaka 2005.
Kifo cha Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mhe. Salmin Awadh Salmin kilitokea jana (19.02.20015) baada ya kuanguka hafla wakati akiwa katika kikao cha kikazi cha Kichama.
Mazishi ya Marehemu Salmin Awadh yalifanyika Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, Wabunge na Wawakishi, viongozi wengine wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, viongozi wa vyama vya siasa,dini na viongozi wastaafu pamoja na wananchi kutoka sehemu mbali mbali nchini.
Mazishi ya Mheshimiwa Salmin Awadh Salmin yamefanywa kwa heshima zote za kichama.
Mapema asubuhi Alhaj Dk. Shein alifika nyumbani kwao maremu huko Magomeni na kwenda kuwahani wafiwa akiwemo kizuka wa marehemu na baada ya hapo aliungana na viongozi mbali mbali katika sala ya kumsalia Marehemu iliyofanyika huko katika Msikiti Noor Mohammad Mpendae.
Akisoma wasifu wa Marehemu, Mkuu wa Utawala wa Baraza la Wawakilishi Amour Mohammed Amour alisema kuwa Marehemu Salmin alizaliwa Juni 6 mwaka 1958 huko Makunduchi, Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja na kupata elimu yake ya msingi katika Skuli ya Kiongozi kuzniz mwaka 1963 na baadae kuendelea na masomo ya Sekondari katika Skuli ya Sekondari ya Makunduchi.
Alieleza kuwa Marehemu Salmin Awadh aliwahi kujiunga na kazi ya Ulinzi kupitia Jeshi la Wananchi JWTZ kuanzia mwaka 1976 hadi 1986 na kufikia cheo cha Sergent. Mbali na kazi hiyo aliwahi kuwa Meneja katika Hoteli ya Narrow Street, Zanzibar baina ya mwaka 2000 na wmaka 2005.
Katika shughuli za kisiasa, marehemu amewahi kushika nyadhifa mbali mbali katika Chama Cha Mapinduzi CCM, ikiwemo Ujumbe wa Halmashauri Kuuu ya Tawi la Magomeni kuanzia mwaka 1982 hadi 1992, Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Jimbo la Magomeni tangu mwaka 1992 na mnamo mwaka 1995 hadi mwaka 2000 marehemu Salmin Awadh alikuwa Diwani wa Magomeni.
Mhe. Salmini alikuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Jimbo la Magomeni Kupitia Chama Cha Mapinduzi tangu uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 na kuendeleaa na wadhifa huo hadi kufariki kwake.
Aidha, Marehemu alichaguliwa kuongoza Kamati mbali mbali ikiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumuya Fedha na Uchumi aya Baraza la Wawakilishi pamoja na Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi Kamati ambayo alikuwa akiiongoza hadi kufariki kwake.
Vile Vile, kutokana na umakini wake na nidhamu ya utendaji kichama mnamo mwezi Juni, 2011Marehemu alichaguliwa kuwa Mnadhimu wa Chama Cha Mapinduzi ndani ya Baraza la Wawakilishi ambapo kwa nafasi hiyo alikuwa pia, Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM, wadhifa ambao ameendelea nao hadi kufariki kwake.
Marehemu Salmin Awadh pia, alikuwa Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na alitoa mchango mkubwa katika Bunge hilo ambapo alikuwa Makamo Mwenyekiti wa Kamati namba 10 ya Bunge hilo.
Aidha, kutokana na uwelewa wake wa masuala mbali mbali Marehemu alichaguliwa kuwa Makamo Mwenyekiti wa Bodo ya Gazeti la Zanzibar Leo kutokea mwaka 2009 hadi kufariki kwake.
Katika kipindi chote cha kuwawakilisha wananchi wa Jimbo la Magomeni, Marehemu alikuwaa mtetezi mkubwa wamaslahi ya wananchi wa Jimbo hilopamoja na wananchi wote wa Zanzibar na aliifanya kazi yake kwa moyo wake wote, uadilifu na mashirikiano makubwa na Wajumbe wenzakwa wa Baraza la Wawakilishi.
Mkuu huyo wa Utawala wa Baraza la Wawakilishi alisema kuwa ni dhahiri kuwa Baraza la Wawakilishi, Chama Cha Mapinduzi, Wananchi wa Jimbo la Magomeni na wananchi wote kwa jumla wameondokewa na mtu muhimu na mahiri mwenye kujiamini katika kusimamia anachokiamini katika kuleta maendeleo ya Taifa.
Marehemu ameacha kizuka na watoto saba. Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi. Amin.
Nae Naibu Katibu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema kuwa Mhe. Salmin amefariki akiwa shujaa ndani ya CCM na kueleza kuwa kauli yake ya mwisho ya marehemu Salmin ni kudumisha chama sambamba na kudumisha Muungano kwani yeye alikuwa muumin wa Muungano.
Nae Mwakilishi wa Kamati ya Wabunge wa CCM alitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya Wabunge hao na kumuelezea marehemu umahiri wake katika kukitumikia chama na wananchi ambapo pia, Kamati hiyo ilitoa Shilingi milioni moja ikiwa ni ubani wa marehemu.
Nao wanafamilia walitoa shukurani kwa Serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa msaada mkubwa walioupata sambamba na mashirikiano katika msiba huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: