Umati wa waombolezaji ulioshiriki kwenye mazishi ya Mke wa Mwanamuziki Mkongwe hapa nchini, Bw. John Kitime, Marehemu Janeth Joan Chidosa Kitime alizikwa jana Februari 16, 2015 kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mume wa Marehemu Janeth Joan Chidosa Kitime, Bw. John Kitime akitoka kuweka shada la maua kwenye kaburi la mkewe wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Watoto wa Marehemu wakielekea kuweka shada la maua kwenye kaburi la Mama yao.
Mfiwa Bw. John Kitime katikati akiwa na Watoto zake mara baada ya Mazishi kwenye makaburi ya Kinondoni,jijini Dar es salaam.
Wadau mbalimbali wakimfariji mfiwa,Mzee John Kitime mara baada ya mazishi kwenye makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es salaam leo.
Dada Nyota Waziri akimfariji Bw. John Kitime mara baada ya mazishi ya mkewe kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Anko Kidevu akimfariji rafiki yake Bw. John Kitime.
Baadhi ya Wanachama wa TBN waliowakilisha kwenye mazishi ya mke wa mwanachama mwenzao, Bw. John Kitime kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam. kutoka kulia ni Cathbert Kajuna, Mkala Fundikira, Jennifer Livigha a.k.a ChingaOne, Ahman na Othman Michuzi pamoja na Muhidin Sufiani.
Toa Maoni Yako:
0 comments: