Na Victor Masangu, Pwani.

Timu ya soka ya Kiluvya united ‘wabishi wa Pwani’ jana iliweza kudhiirishwa umwamba wake katika kandanda baada ya kukata tiketi ya kuweza kupanda ligi daraja la kwanza baada ya kutoka sare ya kufunngana bao 1- 1 na timu ya mshikamano ya Jijini Dar es Salaam huku ikiwa bado na michezo miwili mkononi.

Kiluvya united ambao kwa sasa inashiriki kivumbi cha ligi daraja la pili Taifa ilianza mbio zake za kuwania kupanda daraja tangu mwaka jana ambazo katika muzunguko wa kwanza dalili za kufanya vema zilianz akuonekana kutoka na kikosi cha wachezaji wake kujituma na kushinda katika kila mchezo.

Mchezo wa juzi jumapili dhidi ya wapinzani wao wa timu mshikamano ambao ulipigwa katika dimba la mabatibiti Wilayani Kibaha uliweza kushuhudiwa na umati wa mashabiki ya mshikamano ulikuwa na umati wa mashabiki kutoka sehemu mbali mbali kwa lengo la kuweza kushuhudia nani atakuwa mwamba katika mtangange huo.

Mara baada ya kumalizika kwa mpamabano huo uwanja wote ulilipuka kwa shangwe kutoka kwa mashabiki wa kilivuya united pamoja na wadau mbali mbali kutoka Mkoa wa Pwani pamoja na kutoka nguvu sawa lakini tayari walikuwa wameshajiweka katika nafasi kwani poini walizonazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ile inayoshiriki kivumbi hicho cha ligi daraja la pili.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi pindi mchezo ulipomalizi kocha mkuu wa timu ya Kiluvua united Yahaha Issa Ibdalah alisema kwamba kwa sasa kikosi chake kina jumla ya pointi 20 na kwamba kimabakiza michezo miwili, wakati timu iliyopo nyuma yao ya mshikamo ina juma la pointi 13 ikifuatiwa na abajalo ikiwa na pointi 12 zote za jijini Dar es Salaam.

‘Ndugu mwandishi kwanza kabisa napenda kumshukuru mungu kwa timu yangu kupanda daraja la kwanza nah ii yote nikutokana na juhudi za wachezaji uongozi mzima wa kiluvua united, pamoja na mwamko wa mashabiki wa kiluvua na Pwaniu kwa ujumla lakini kwa sas sisi ndio kinara kwani tuna pointi 20 na bado tuna mechi mbili dhidi ya Abajalo pamoja na Cosmo hivyo hakuna timu yoyotre ile ambao itaweza kufikia pointi zetu haya kama wakishinda mechi zote,”alifafanua Kocha Issa.

Kocha huyo ambaye mafanikio yake yameanza kuonekana tangu miaka ya nyuma iliyopita kutoka ana uwezo wake aliokuwa nao ambapo alishaipeleka timu ya kiluvuya united hadi kuwa mabingwa wa Mkoa wa Pwani mara mbili kitu ambacho kiliweza kumuongezea sifa lukuki kutoka wa mashabiki na wadau wa mchezo wa kabumbu kwa Mkoa wa Pwani na Taifa kwa ujumla.

Kadhalika akifafanua zaidi kuhusiana na uzoefu wake katika kulisukuma gozi kucho huyo amebainisha kuwa alishwahi kuchezea katika timu mbali mbali ikiwemo Lipuli,Bandari ya Dar es Salaaam, Kawe Ranger, Takoshili,Pan Afrika, Reli,Moro united, Temeke United, Yanga Afrika watoto wa jangwani pamoja na timu nyinginezo za nje ya nchi ikiwemo Rwanda.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa timu hiyo ya Kiluvya United, Edward Mgogo “Eddo Master” alisema kwamba ndoto yao kubwa ni kuhakikisha timu hiyo inafika mbali ili kuweza kushiriki katika ligi kuu ya Tanzaania bara.

Aidha alitoa wito kwa wadau mbali mbali na mashabiki wa Mkoa wa Pwani kuipa sapoti ya kutosha timu hiyo ili kuweza kutimiza azama yao ya kuweza kufika mabli na hatimaye katika siku zijazo iweze kushiriki hata michuano mbali mbali ya Kimataifa.

Kikosi hicho ambacho kwa sasa kimeacha gumzo ya hali ya juu kutokana na wachezaji wake kuonyesha kandanda la aina yake siku ya jumamosi kinatarajia kushuka dimbani kumenyana na timu ya Abajalo katika nyasi za uwanja wa Karume Jijiji Dar es Salaam ikiwa kama kumalizia michezo yake miwili ya mzunguko wa mwisho.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: