Niliporudi nyumbani, mume wangu akasema anaomba tutumie gari moja tu, moja tupaki, atakuwa ananipeleka kisha ananirudisha, nilirukia haraka nikamwambia sitaki, na nikamuuliza kuna maana gani ya kuwa na magari mawili nini? ulinunulia la nini wakati ulijua unaweza kunipitia, akasema nimeamua tu, mke wangu nini shida kwani?, wewe nakupeleka nakurudisha kama una issue zako nitakupeleka nakuacha ufanye mimi naondoka badaae nakufata... ilibidi nikatae na yeye akasema sawa.
Usiku ulipofika kazi ilikuwa ni kazi kusema kweli sikuwa na hisia zozote juu yake mimi nilikuwa namuwaza Kelvin tu, nikamuuliza kuna shida gani akasema hakuna shida yeyote. Alipomaliza hakusubiri nimsafishe alinyanyuka kitandani na kwenda kuoga.
Nakumbuka wakati nipo na mume wangu mwanzo maandalizi katika malavidavi yalikuwa moto sana kadili tulivyokuwa tunaenda akawa anaacha hata kunibusu kimoyo moyo nikajiuliza sijui ameshagundua kama nimeshaanza mahusiano na Kelvin
Mahusiano yangu na Kelvin wale marafiki zangu waliyajua vizuri sana, siku ya kuadhimisha siku yangu ya kuzaliwa (bithdday) nilipotoka nikamkuta Kelvin ananisubiri nje ya nyumba yetu na akanichukuwa kunipeleka hotel moja hivi iko Sinza, Dar nzuri sana nikakaa kama nusu saa wakaja marafiki zangu na na keki... nilibaki nashagaa, nikiwa hapo mme wangu alinipigia simu kuuliza niko wapi... nikakimbilia chooni kupokea simu, akauliza uko wapi mama???, nikasema Muhimbili nimekuja kumuona mama yake rafiki yangu anaumwa, akasema mbona sauti ina mwangwi, na kumetulia hivyo, nikasema niko chooni nakojoa, akasema mbona hukuaga, nikasema sorry, ilikuwa urgently,… alichosema ni kimoja tu,,, KUWA MAKINI NA MAAMUZI UNAYOTAKA KUYAFANYA, akakata simu.
Nilikaa hapo bila hofu kabisa mbaya zaidi nikisema nawahi nyumbani kwa mume wangu hapo marafiki zangu wakaniuliza unamnyonyesha? Kaa ule raha hapa,,,, nilikaa kweli hadi saa mbili, nikiwa hoi, akawa ameanza kunipa pombe ninywe, nilishindwa kwakweli nikaanza kunywa wine tu ambazo nazo sikuwa nikitumia zamani, siku hiyo Kelvin alipenda tufanye mapenzi ili iwe zawadi kwake na alitaka watakapoondoka marafiki zangu na kweli alifanikisha dhamira yake.
Nilikaa nae kwa muda mchache na kurudi nyumbani, wakati naingia na gari nyumbani namkuta mme wangu kakaa kibarazani ila kaka wa getini wakati ananifungulia mlango aliniambia, dada leo shemeji ana hasira sana... sijui kwanini, (kijana wa getini ni ndugu yangu hivyo yuko huru kwangu) nikamuuliza kakuulizaje? akasema aliniambia ikifika saa nne haujafika nisifungue geti atakuja kukufungulia yeye.
Nyumba yetu niya ghorofa ile naingia getini naongea na mlinzi kumbe mume wangu yuko ghorofani ananiangalia japo mimi sikumuona maana ilikuwa ni usiku alikuwa amekaa kwenye kona, baadae ndiyo kaka akaniambia umeona anavyokuangalia yule kule juu, ndipo nikamuona, alipogundua nimemuona tu akarudi ndani haraka... ile naingia sebuleni nae anashuka ngazi, akanifata akanikumbatia akasema nikupoke pochi... kisha twende dining kuna zawadi yako hapo nikapata hofu tukaenda hadi dining, nikakuta kuna keki, akamuita dada aandae sahani alete cha champagine, basi nikajikausha kama sio mie nikafurahi ili awe na Amani.
Nikashangaa mbona hasira nilizoambiwa anazo sizioni tena?? nilibaki na viulizo akilini. Basi tukakata keki tukala, wakaniimbia wote na kina dada na kaka wa mlangoni kisha wakasambaa, tukapanda juu kulala, ile nafika juu tu akaniambia anazawadi nyingine njoo tukae hapa tuongee kidogo nikupatie zawadi.
Akaniomba tukae sebule ya juu, ambayo inatazamana na chumba chetu nikamwambia nisubiri basi nakuja. Basi niliingia ndani nikachukua simu nikamtumia meseji Kelvin asinipigie maana nimefika nyumbani, hakujibu chochote kile, basi nilitoka nje nikakaa sebuleni na taulo langu, mme wangu akasema mbona hukuniaga ulipoenda na sio kawaida yako??? Akasema mbona hukuniambia wakati huwa unaaga, nikamwambia mgonjwa alizidiwa nikachanganyikiwa akasmea,,, KUWA MAKINI NA HAYO UNAYOTAKA KUYAFANYA, akanifata akaniambia nakupenda sana, jitahidi uniheshimu, usiniumize, nikasema sawa, akaniambia, chukuwa zawadi yako pale kwenye kabati la vitabu.
Nikaenda nikakuta simu nzuri ya HTC ONE rangi ya gold, Niliruka sana nikamkumbatia, akafurahi akaniambia basi furaha iendelee pale sebuleni... sikujivunga nafuraha ya simu nikampa ila kuna kitu alihisi, maana alipoanza tu kazi nikaona kaniangalia usoni na akakosa furaha.
Endelea kufuatilia sehemu ya tatu... itawajia kesho....
Toa Maoni Yako:
0 comments: