Mmmmhh! Miaka saba leo imefika kama mchezo!!!!

Hapa nipo nyumbani Songea/Ruhuwiko katika shughuli za kuandaa madikodiko nikiwa na wifi yangu tukisaidiana na pembeni ni kakangu mdogo. Ilikuwa inakaribia mwaka mpya 2015.

Blog ya Maisha na Mafanikio kama mchezo leo yatimiza miaka saba (7) kamili. Napenda kuchukua nafasi hii na kusema:- Hii yote ni kutokana na uwepo wenu ulioambatana na upendo pia ushirikiano mzuri mlio nao. Na kubwa zaidi ni kwa familia yangu kwa kuwa bega kwa bega nami.

Pia napenda kusema kwa kupitia michango ya wasomaji na wanablog wenzangu nimeweza kijifunza mambo mengi sana. Na ndiyo kwa sababa hii napenda kusema:- AHSANTENI SANA KWA USHIRIKIANO WENU NASEMA TENA KWANI NAAMINI BILA NINYI, NISINGEFIKA HAPA NILIPO LEO. KWA KWELI NAAMINI KUWA SISI SOTE NI NDUGU NA NI WATOTO WA BABA MMOJA. UPENDO NA UMOJA WETU UDUMU DAIMA NA PIA MILELE!!!!!..........

Imetolewa na 

Yasinta Ngonyani
Mmiliki wa Blog ya Maisha na Mafanikio

Zaidi na zaidi unaweza kumtembelea hapa... http://ruhuwiko.blogspot.com/
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: