Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Julieth Kairuki akiongea katika hafla ya pamoja baina ya Kampuni zinazojiushisha na utengenezaji wa vifaa vya umeme MCL ya Tanzania na KDK ya Japan kuingia makubaliano yatakayosaidia usambazaji wa vifaa vya umeme hapa nchini.

Na Mwandishi Wetu.

SERIKALI imesisitiza azma yake ya kuendelea kuwaunga mkono wawekezaji wanaokuja nchini kwa lengo la kuwekeza na hiyo ni kutokana na umuhimu wao ukiwemo wa kuzalisha ajira kwa wananchi pamoja na kuchangia pato la Taifa kwa kulipa kodi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Julieth Kairuki wakati wa hafla ya pamoja baina ya Kampuni zinazojiushisha na utengenezaji wa vifaa vya umeme MCL ya Tanzania na KDK ya Japan kuingia makubaliano yatakayosaidia usambazaji wa vifaa hivyo hapa nchini.
 Mkurugenzi wa kampuni ya MCL, Murtaza  Alibhai akizungumza katika hafla ya pamoja baina ya Kampuni zinazojiushisha na utengenezaji wa vifaa vya umeme MCL ya Tanzania na KDK ya Japan kuingia makubaliano yatakayosaidia usambazaji wa vifaa vya umeme hapa nchini.

Meneja Ufundi wa Kampuni ya MCL, Dennis Rungu akizungumza machache juu ya ubora wa bidhaa za MCL.
Mshereheshaji Gadner G. Habash akiendesha  hafla hiyo.
Wakizindua bidhaa za MCL na KDK.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya MCL, Murtazah Alibah amesema makubaliano ya ushirikiano yaliyofikiwa na baina ya MCL na KDK yanalengo la kuboresha upatikanaji wa vya umeme katika soko la hapa nchini vyenye viwango bora.

Aidha MURTAZAH amesema imani yake watanzania watanufahika kupitia ushirikiano huo huku akizitaka mamlaka zinazohusika na ukaguzi vifaa hivyo kuzidisha ukaguzi wake ili kuondoa bidhaa feki zilizopo mitaani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: