Ni kweli mimi ni Albino, nimejikubali na nimeishi maisha yangu yote bila kujali nilivyo. Sijawahi kutumia hali yangu kupata kitu kwa huruma, nimeyapigania maisha yangu na nimepiga hatua.

Leo hii naongea nanyi nikiwa Baba, Mume, Mwandishi Mwandamizi, Blogger, na mengine mengi, lakini hali yangu sasa inaanza kunikwaza.

Haya mauaji jamani, nimejiteua kuwa Balozi, nitatetea, na kusimama mbele ya wenzangu wote wenye hali kama hii, kama ni wanasiasa ama wafanyabiashara, wanataka kutuua kwa maslahi binafsi, mwaka huu HAPANA.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: