John Massawe alikuwa kanisani, kapu la sadaka likaanza kupitishwa, lilipofika kwake akatoa noti ya shilingi mia tano akaikunja kisirisiri akaitumbukiza kwenye kapu.
Mara ile ile akaguswa begani na mtu aliyekuwa nyuma yake, kugeuka akakuta jamaa anampa noti mbili za elfu kumi, akajua jamaa anataka kutoa sadaka, akazipokea na na kuzitia katika kapu.
Walipomaliza ibada tu Massawe akamfuata nje yule mheshimiwa aliyetoa shilingi elfu Ishirini (20,000/=), na kuanza kumpa hongera kwa kujitolea fungu kubwa vile katika sadaka. Mheshimiwa akajibu,’Hapana haikuwa sadaka yangu, ulipokuwa unatoa sadaka yako mfukoni, zile hela zilidondoka kutoka kwenye mfuko wako, nikaziokota na kukurudishia.
Massawe akapiga ukunga "yele uwiiiiiii, Yesu na Maria" akamfuata mchungaji ili amrudishie elfu ishirini (20,000/=) yake, akajibiwa imeshakabidhiwa kwa Mungu jamaa akaanguka akazimia.
Watu wakampeleka hospital, alivyozinduka akakuta yupo na dada mwenye nguo nyeupe akamwambia "afadhali nimekuona Malaika naomba mwambie Mungu anirudishie hela yangu niliitoa kimakosa kanisani "dada akamjibu mimi ni Nesi na hapa sio kwa Mungu ni hosipital. Massawe akazimia tena.
Toa Maoni Yako:
0 comments: