Rais wa Brazil wa mrengo wa kushoto Dilma Rousseff ametoa wito wa kuimarisha umoja baada ya kupata ushindi mdogo hapo jana, unaompa ridhaa ya kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa pili.
Rousseff, mwanamke wa kwanza kuongoza taifa la saba kwa ukubwa kiuchumi, alipata kura asilimia 51.64, huku mpinzani wake Aecio Neves akiambulia asilimia 48.36 baada ya kuhesabiwa zaidi ya asilimia 99 za kura.
Toa Maoni Yako:
0 comments: