Mwanamuziki wa zamani na mbunge Vicky Kamata baada ya ndoa yake kudaiwa kuzuiliwa kufungwa kutokana na kudaiwa mwanaume aliyetaka kufunga naye ndoa ana ndoa nyingine, amefunguka kwa kudai kuwa hizo zilikuwa ni habari za kutungwa na hazikuwa na ukweli wowote.

Vicky ameiambia amplifaya ya Clouds fm jana kuwa maneno mengi ambayo yalikuwa yanazungumzwa kuhusu ndoa yake kutofungwa yalikuwa yametengenezwa na watu.

“Kweli ni maradhi kama ambavyo ilitangazwa wakati huo, lakini pamoja na hayo mimi bado nasema Mungu alikuwa hajapanga, alikuwa hajaruhusu kuwa tarehe 24 mwezi wa tano iwe siku wa kufunga ndoa.

“Mimi kama binadamu na mwenzangu tulipanga lakini Mungu alipanga vinginevyo, kwahiyo siku zote mapenzi ya Mungu huwaga yanatimia siyo mapenzi ya binadamu.

“Ni kweli alishawai kufunga ndoa lakini ninachofahamu mimi ni kwamba waliachana kihalali kabisa kwa divorce ya mahakama ya Kinondoni jijini Dar mwaka 2012 na mimi siyo mtoto mdogo kwamba ninaweza mpaka nikafikia hatua hiyo bila kuwa nimemchunguza huyo mtu.

“Kuhusu swala la kwamba alikuwa na mke wake, mke wake alikwenda kuzuia Kanisani sijui alikuja Bungeni, yale yalikuwa tu ni maneno ambayo yalitengenezwa na baadhi ya watu kwa interest zao, lakini siyo kwamba nilikuwa nimeingilia ndoa ya mtu hata kidogo, kwa sababu ata huyo mke wa kwanza wa huyo aliyekuwa mchumba wangu aliongea na vyombo vya habari akasema mimi sijaenda Dodoma wala sijaenda kuzuia harusi.

“Kwahiyo maneno yaliyokuwa yamezagaa, sijui mke wake amezuia yalikuwa ni maneno ya kutengenezwa na watu tu kwa nia zao wenyewe lakini siyo kweli.

“Kuhusu kwamba hajulikani alipo mimi hilo siwezi kumjibia, mimi nafahamu kwamba yupo na anaendelea na shughuli zake kama kawaida, kama ambavyo mimi naendelea na shughuli zangu kama kawaida, tunawasiliana, yani cha kufahamu tu kwamba ndoa haikufungwa basi.

“Hata kama kuna mkono wa binadamu katika jambo hilo mimi naamini Mungu ndio mwenye mamlaka na Mungu ndiyo mwenye kupanga mambo, kwahiyo kama Mungu alikuwa anataka hiyo harusi ifugwe ata kama kungekuwa na binadamu mwingine hataki bado ingefungwa.

“Mimi sitaki kuamini sana kwamba kuna waheshimiwa wabunge wenzangu wamechangia kwa kiasi kikubwa kwamba ndoa ile isifungwe, mimi ninaamini ni mapenzi ya Mungu tu yametimizwa kwa staili hiyo” Alisema Vicky
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

3 comments:

  1. Hiyo ndoa itakuwa feki labda asubili mpaka mke wa huyo anaedai yeye ni mchumba wake afe au atafute ndoa ya kiislam awe mke wa nne au wa pili
    Na pia awe bayana asifiche ukweli

    ReplyDelete
  2. Atafute ndoa ya kiislam haina taabu wala haina pingamizi au asubili sana mpa mke wa huyo mchumba wake afe kisha yeye aolewe hapo hatapata ugonjwa tena na ndoa itafanyika

    ReplyDelete