Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mhe. Joshua Nassari kesho anatarajia kufunga ndoa na Bi Anande Nko katika kanisa la Pentekoste, Kilinga lililoko wilaya ya Meru ambako Mheshimiwa Nassari alianzia masuala ya Kiimani ikifuatiwa na Sherehe kubwa ya Harusi itakayo fanyika katika viwanja vya Usa - River Academy jirani na Hotel ya Ngurdoto.

Kwa Mujibu wa Mh Nassari, sherehe hizo zitakazoanza majira ya saa saba mchana watu wote wamealikwa wakiwemo ndugu, marafiki, Jamaa na wananchi jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tukio hilo na kamba hakuna kadi.

"Nichukue tena fursa hii kuwakaribisha ndg, marafiki, Jamaa na zaidi sana wananchi wangu wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tendo hadhimu la kusherekea harusi yangu , Jumamosi Juni 7, Usa-River academy grounds kuanzia saa saba mchana. Kwa Pamoja Tulianza na Mungu, Tutamaliza na Mungu Pamoja. ...No cards on entrance!"alisema Nassari.

Nassari amesema watu zaidi ya 8000 wanatazamiwa kushiriki katika sherehe hiyo ya aina yake wakiwemo viongozi mbalimbali na wabunge kutoka maeneo mbalimbali.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: