Mabalozi wa Huduma mpya ya Airtel ya ‘SWITCH ON’ Wasanii Ney wa Mitego, Vanessa Mdee na Barnabas wakiwa wameshikilia mabango yenye kuonyesha namba ya kujiunga na huduma hiyo ya intaneti wakati wa hafla ya uzinduzi wake ilifanyika juzi usiku katika Hoteli ya Hyatt Agency - The Kilimanjaro, Jijini Dar es Salaam. 

Msanii maarufu kwa kumiliki jukwaa na balozi wa huduma ya Airtel ya ‘SWITCH ON’ Vanessa Mdee akiwa na wacheza shoo wakitoa burudani kali kwa wageni waalikwa  waliohudhulia hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel kwa watumiaji wa Internet hapa nchini ijulikanayo kama SWITCH ON. 

Waandishi wa Habari toka vyombo mbali mbali wakiwajibikawakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel kwa watumiaji wa Internet hapa nchini ijulikanayo kama SWITCH ON. 
 Wageni waalikwa wakijadiliana mawili matatu.
 Show love za hapa na pale...
 Kila mmoja akiwa ame ‘SWITCH ON’
 Wageni waalikwa wakishow love...
Balozi wa huduma ya Airtel ya ‘SWITCH ON’ Msanii Ney wa Mitego akitoa burudani. 
 Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel imezindua huduma kabambe ya Intaneti itakayojulikana kama SWITCH ON. Huduma hiyo ni maalum kwa watumiaji wa huduma za Interneti Tanzania ambapo sasa wateja wa Airtel wataweza kufuruhai huduma ya kipekee ya vifurushi vya data/intaneti maalum kwa simu na mahitaji ya kila mteja.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania Bw, Levi Nyakundi alisema “ ulimwengu wa leo matumizi ya huduma za intaneti/data au mtandao hayaepukiki, ukitaka kujua kinachoendelea duniani kwa haraka basi intaneti ndio suluhisho au jawabu linapopatikana, lakini kumekua na changamoto nyingi sana hasa pale tunapohitaji intaneti bora ya kutuwezesha kufanya fasta mawasiliano na tuwapendao au tunapotaka kuunganishwa na taarifa za mambo muhimu yanayoendelea dunia kote, inawezekana kila wakati umekua ukijiuliza ni MB au GB au kifurushi gani kitakuwezesha kufanya mambo yako kuwa poa zaidi, hili ndilo lililotusukuma Airtel kukuletea wewe mteja wetu huduma hii ya kisasa na ndio maana tunakuambia SWITCH ON”

“Ukiwa na Airtel ‘SWITCH ON’ watumiaji wa huduma za Intaneti Tanzania sasa wanakila sababu yakufurahia kujipatia huduma bora zaidi kwa gharama nafuu na kufanya chaguo la kufurushi utakacho MAALUM kwa simu yako.

Hii ni huduma inayoenda na wakati, inazingatia utamaduni wetu kwa kuwa ni ya kukutoshelezea hitaji lako, na gharama ni nafuu kuliko zote huku ikikuhakikishia mteja Non-stop intaneti - yaani fulu makamuzi kwa wewe mtumiaji kutokupimiwa. Huduma hii ya pia inamuwezesha mteja kuwa na chaguo la kifurushi iwe kwa SIKU, WIKI au MWEZI”.
Mkurungenzi wa Kajunason Blog, Cathbert Kajuna (kushoto) akiwa na Mwandishi wa Habari wa BBC ambaye yupo nchini Tanzania, Noel Mwakalindile
Mkurungenzi wa Kajunason Blog, Cathbert Kajuna (kulia) wakijadili jambo na Mkurugenzi wa Michuzi Media Group, Othman Michuzi na mwenzake wakati wa hafla ya uzinduzi wake ilifanyika juzi usiku katika Hoteli ya Hyatt Agency - The Kilimanjaro, Jijini Dar es Salaam.
 Dj Choka akiidadavua simu aina ya Samsung S5... pembeni ni Mtangazaji wa Clouds Fm, Hamis Mandi.
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania Bw, Levi Nyakundi akiongea machache katika uzinduzi huo.
Burudani ya kutosha ilikuwepo...
Mabalozi wa Huduma mpya ya Airtel ya ‘SWITCH ON’ wasanii maarufu Ney wa Mitego, Vannessa Mdee na Barnabas wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi.
Wadau toka Clouds Fm, Jimmy Jam na Kibonde.
Furaha na bashasha zilitawalaaaaa...
Wafanyakazi wa Airtel wakishow love.
 Mambo ya duania... mwanadada aliyeamua kuweka headline kwa kuvaa nguo iliyoacha wazi upande mmoja wa mwili wake.. hii inaitwa kAniTAnGaZE


Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akitoa zawadi a simu.
Mwanadada Miss Popular alikuwa ni miongoni mwa watu waliojipatia zawadi ya simu siku ya uzinduzi.

“Airtel Tanzania tumejipanga zaidi kuhakikisha tunaendelea kuwa wabunifu na kuwapatia huduma bora ya mawasiliano ya internet. Tutaendelea kufanikisha hili kwakuwa Airtel Yatosha, Airtel Money nusu gharama, au Bure Pack ni vielelezo vya huduma bora na nafuu tunazowapatia wateja wetu kwa sasa na kuwafaidisha wateja kila siku. Hivyo leo hii SWITCH ON nimuendelezo wa kuwahudumia watumiaji wa Internet nchini Tanzania kwa kuwapa wanachokitaka bila kikwazo yaani Fulu makamuzi” aliongeza Nyakundi.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Airtel Bi Prisca Tembo akielezea jinsi ya kutumia huduma hiyo alisema “Ni rahisi sana mteja wetu kujiunga, unatakiwa tu kupiga *148*22# ikiwa tu una simu yako yenye uwezo wa kutumia intaneti /Data kisha utaweza kujichagulia aina ya kifurushi kinachokufaa kutokana na mahitaji yako kwa kuwa vifurushi ni maalum kwa simu au kifaa utakachotumia yaani iwe unasimu ya Feature phone, au Simu mpapaso (Smart phone au Tablet sisi Airtel tumekuwekea kifurishi cha intaneti maalum kwa kila simu”

‘Vilevile kwa wale wateja wote wa Airtel wanaotumia huduma ya Airtel Yatosha pia bado wananafasi ya kujiunga na vifurushi vya intaneti vya Yatosha na ikiwa wamemaliza Data /intaneti na wanapenda kujiunga na Data pekee basi wanaweza pia KU-SWITCH ON na kuendela na makamuzi” alimalizia kusema Prisca
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: