Mwanamuziki Hamis Mwinjumah akiongea na mashabiki wa muziki wa mkoa wa Kilimanjaro, kupitia Redio ya Kili FM 
---
Na Mwandishi Wetu, Moshi.

Ziara ya Kilimanjaro Music Tour ambayo ndio gumzo kubwa sasa katika sekta ya burudani imebisha hodi katika Mji wa Moshi ambapo wapenzi wa muziki wanatarajiwa kupata burudani ya aina yake kutoka kwa wasanii mbalimbali Jumamosi hii.

Maandalizi yote yamekamilika huku zaidi ya wasanii 10 wa humu nchini wameshatua mjini tayari kwa show kubwa itakayofanyika katika Viwanja vya Chuo Shirikishi cha Ushirika na Biashara (MUCCOBs).
Mwanamuziki Ommy Dimpoz naye akiongea na mashabiki wa muziki wa mkoa wa Kilimanjaro, kupitia Redio ya Kili FM 

Ziara hii inadhaminiwa na Bia ya Kilimanajro Premium Lager ambayo imekuwa mstari wa mbele katika kufikisha muziki wa Tanzania kwenye kilele cha mafanikio. Ziara hii inaratibiwa na EATV na East Africa Radio, Executive Solutions, Integrated na AIM.

Wasanii watakaotoa burudani ni pamoja na Ommy Dimpoz, Kala Jeremiah, Weusi, Ben Pol, Jambo Squad, Young Killer, Ney wa Mitego, Mwana FA, Khadija Kopa, Warriors na Professor J.
PICHANI JUU NA CHINI: Mandhari ya eneo la tukio kama yalivyoone

“Wasanii wote wako tayari kutoa burudani ya aina yake na sisi kama wadhamini tunawaahidi wakazi wa Moshi mambo mazuri... waje kwa wingi wakutane na wasanii wao na pia wapate burudani bila kusahau Bia yao namba moja Kilimanjaro Premium Lager,” alisema Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe.

Alisema kiingilio katika show hii itakayoanza saa nne asubuhi ni Tsh 2,500 na kila atakayeingia atapewa bia ya bure mradi ametimiza umri wa miaka 18.

Tiketi wa ajili ya show hii zimeshaanza kuuzwa leo Ijumaa MUCCOBs na pia promosheni mbalimbali za kusisimua zinaendelea katika baa tofauti Mjini Moshi.
“Ziara hii sio ya washindi wa Tuzo za Muziki (Kilimanjaro Music Awards) bali ni ziara ya wasanii ili waweze kutangaza kazi zao pamoja na kupeleka burudani mikoani ili watu wanaokaa huko pia waweze kufaidi,” alisema Bw Kavishe.


Aliongeza kuwa wasanii wana nafasi kubwa sana kueneza ujumbe mbalimbali katika jamii hivyo wanapaswa kuungwa mkono ili waweze kuwafikia wananchi wakiwemo wa mikoani.

Ziara hii itahusisha mikoa ya Moshi, Mwanza, Kigoma, Kahama, Iringa, Mbeya, Dodoma, Tanga, Mtwara na Dar es Salaam na inaanzia Mkoani Moshi Mei 24, Mwanza Mei 31, Kahama Juni 7, Kigoma Juni 14, Iringa Juni 21, Mbeya Agosti 9, Dodoma Agosti 16, Tanga Agosti 23, Mtwara Agosti 30, Dar es Salaam Septemba 6,” alisema Kavishe.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: