Rais TFF,  Mh Jamal Malinzi na Mwenyekiti wa makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza wakitia saini katika mkataba wa makubaliano ya udhamini wa ligi ya mpira wa miguu kwa wanawake itakayoanza mwezi wa Nane.
Raisi wa TFF, Mh Jamal Malinzi (kushoto) akibadilishana mkataba wa udhamini na Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza (katikati) mara baada ya kumaliza kutiliana saini katika mikataba hiyo mbele ya waandishi wa habari leo katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Southern Sun. Anayeshuhudia pembeni ni Katibu wa Michezo kutoka Kampuni ya Proin, Godlisten Anderson.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Cha Wanawake, Bi Lina Muhando akiongea na Waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Sourthen Sun wakati Kampuni ya Proin ilitangaza kudhamini ligi ya wanawake inayotarajiwa kuanza Mwezi wa Nane.
Rais Wa TFF, Mh Jamal Malinzi akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kuweka saini katika Mkataba wa Udhamini kati ya Proin Promotions na TFF.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: