Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mkoani Dodoma Betty Mkwasa, akiongea na Wananchi wa kijiji cha Chipanga kabla ya kupokea msaada wa vitanda kwa ajili ya zahanai ya kijijini hapo vilivyotolewa na Vodacom Foundation kuboresha huduma za afya kwa mama na mtoto.
Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Chipanga wakisaidia kubeba vitanda vya msaada vilivyotolewa na Vodacom Foundation kuvipeleka katika wodi ya akinamama tayari kwa ajili ya matumizi.Vitanda hivyo vilikuwa na thamani ya Sh 10 Milioni .

Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma Betty Mkwassa (wa ttau kushoto) akipokea moja ya vitanda 9 kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kati Mruta Hamisi vilivyotolewa na mfuko wa kampuni hiyo wa kusaidia jamii (Vodacom Foundation) kwa ajili ya wodi ya wanawake katika kituo cha afya cha kijiji cha Chipanga.Kampuni ya Vodacom imejikita katika kusaidia uboreshaji wa huduma za afya hasa kwa wanawake na watoto chini ya mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii.
Mama mjamzito Vailet Petro (katikati) mkazi wa kijiji cha Chipanga, Wilaya ya Bahi Dodoma akimwaga chozi la furaha mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo Betty Mkwassa (kushoto) na Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kati (kulia) baada ya kushuhudia kituo cha afya cha kijini hapo kikipokea vitanda tisa kutoka Vodacom Foundation kwa ajili ya wodi ya wanawake. . Msaada huo umewaondolea adha akina mama ambao walikuwa wakilala sakafuni kutokana na uhaba mkubwa wa vitanda uliokuwa ukikikabili kituo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Betty Mkwassa (katikati) akiteta na Mkuu wa Vodacom kanda ya kati Mruta Hamisi wakati walipokuwa wakimjulia hali mzazi aliyejifungua katika kituo cha afya Cha Chipanga wilayani Bahi.Kituo hicho huhudumia wakazi wa Bahi mkoa wa Dodoma na Manyoni mkoani Singida. Vodacom Foundation imekabidhi vitanda 9 vya wagojwa kwa ajili ya wodi ya wanawake yenye uhaba mkubwa wa vitanda.

Na Mwandishi Wetu, DODOMA.

Kituo cha Afya cha Chipanga, kilichopo Bahi mkoani Dodoma kimepokea msaada wa vitanda tisa vilivyotolewa na Mfuko wa kusaidia jamii wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom (Vodacom Foundation) lengo likiwa ni kuwapunguzia changamoto wazazi na watoto wanaopatiwa huduma kituoni hapo.
Kituo hicho, mbali ya kuwa kijijini, ndio tegemeo la huduma za afya kwa wakazi wa wilaya ya Bahi na Manyoni ya Mkoani Singida hivyo kuifanya kuwa na uhitaji mkubwa.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kati Mruta Hamis, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Bi. Betty Mkwasa ameishukuru kampuni hiyo kwa kuona adha waliyokuwa wakiipata kinamama wajawazito wa kijijini hapo na kuamua kuwapatia vitanda hivyo.
Amesema kutokana na kuhudumia wiyala mbili, kituo hicho cha afya kimejikuta kikiwa na uhaba mkubwa wa vitanda kwenye wodi ya wazazi ambao hupata huduma ya kujifunua kituoni hapo ikiwemo kwa njia ya upasuaji.

“Tunashukuru sana Vodacom kwa namna ambavyo mmekuwa mkiiunga mkono jamii inayo wazunguka, kina mama wa kijiji hiki wamekuwa wakilala chini kwa muda mrefu, kupatikana kwa Vitanda hivi ni faraja kubwa kwao,” Alisema Mkwasa na Kuongeza.

“Leo wote tunafuraha hapa hasa akina mama, ili furaha hii idumu na tuwaoneshe Vodacom kwamba walichotupatia ni kitu tulichokuwa tukikihitaji sana, ni vema wote kwa umoja wetu tuhakikishe tunavitunza vyema vitanda hivi, ili viweze kudumu kwa muda mrefu na visiturudishe nyuma, kinyume cha hapo taturudi kule tulikotoka kulala sakafuni ambako naamini tayari pamshakuwa historia kwa msaada wa Vodacom Foundation.”

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa makampuni hususan yaliyo katika sekta binafsi kuendelea kuwekeza katika jamii inayowazunguka katika kuimarisha ubia kati ya serikali na sekta binafsi kwa lengo la kuboresha na kustawisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi ikiwemo huduma za afya na elimu..

“Serikali inathamini na inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi kama huu unaofanywa na Vodacom ambayo imekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii inayowazunguka kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili, huu ni ubia wakupigiwa mfano na kuigwa na kila kampuni ili kuiwezesha serikaai kuwafikishia huduma za kijamii wananchi.”

Aidha, kufuatia msaada huo utakaowasaidia wakina mama wajawazito kujifungulia kwenye vitanda, Halmashauri ya wilaya ya Bahi kupitia kaimu mganga mkuu wake, Dk. Gerald Maro, imeahidi kutoa magodoro tisa, ili vitanda hivyo vianze kutumika mapema iwezekanavyo.

“Vodacom wamefanya kazi kubwa ya Kutufikishia Vitanda hivi sisi kama Halmashauri tunaahidi kununua magodoro ya Vitanda hivi mapema ili viweze kutumika na mama zetu waweze kujifungulia mahali Salama” alisema Dk. Maro.

Kwa upande wao, uongozi wa kituo hicho cha afya cha Chipanga, kupitia kwa Mganga mfawidhi, Dk. Majegenja Sirira, kimetoa shukran zake za dhati kwa Vodacom, kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.

Kutolewa kwa msaada huo, kumeelezewa na uongozi wa kituo hicho cha afya utapunguza kwa kiwango kikubwa uhaba wa vitanda, ikizingatiwa kuwa kituo hicho chenye chumba cha upasuaji, kimekuwa kikitoa huduma kwa wilaya mbili, bahi iliyopo mkoani Dodoma na Manyoni, iliyopo mkoani Singida.

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kati, Bw. Hamis Mruta, amesema Vodacom kupitia mfuko wake wa kusiadia Jamii wa Vodacom Foundation inatambua na kuthamini umuhimu w akuwekeza kwa jamii za mjini na vijijini.

Amesema Vodacom Foundation imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kusaidia kupunguza changamoto za kijamii hasa kwenye upatikanaji wa huduma za afya,elimu na uwezeshaji wananchi hususan wanawake ikiunga mkono juhudi za serikali na wanajamii wenyewe za kuhakikisha huduma hizo zinzpatikana kwa ubora na urahisi.

“Tunachokifanya leo ni mwendelezo wa dhamira yetru ya kusiadai jamii kwa kuhakikisha inaondokona na changamoto na hatiame kuwawezesha kubadili maisha yao.”Alisema Mruta

Amesema ahadi ya Vodacom kwa watanzania ni kwamba itaendelea kusaidia jitihada za serikali za kuwapatia wananchi huduma bora za kijamii kwa kutoa kipaumeble katika huduma za elimu na afya.

“Leo tunawapatia furaha na tabasamu mama zetu tukiamini kuwa sasa mnapo mahala salama na penye staha pakujifungulia na hata pakupokea huduam bora zenu na za watoto.”Aliongeza Mruta.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: