Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini inapenda kukanusha kuhusiana na taarifa ya ujumbe mfupi wa simu na katika mitandao ya kijamii wenye maneno yafuatayo : ‘TMA warning heavy rains of strong easterly winds 100km an hour expected to hit Dar coast from Somalia, Heavy rains 120mm above sea level expected today and tommorrow. People must avoid Sea and areas near to Sea should be alert cautioned. Tanzania Meteorological Agency www.tma.gov.tz’

Mamlaka inapenda kuutaarifu umma kuwa taarifa hiyo siyo ya kweli na ina lengo la kupotosha umma na wala haijatolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

Mamlaka ina kuwakumbusha wananchi wote kuendelea kufuatilia taarifa zetu kupitia vyanzo husika vya Mamlaka vikiwemo utabiri wa kila siku utolewao kupitia radio, televisheni na tovuti ya Mamlaka (www.meteo.go.tz).

Taarifa sahihi za mwenendo wa mvua na tahadhari za hali mbaya ya hewa zinatolewa na zinapatikana kupitia njia rasmi za utoaji taarifa maalum za kiofisi (official weather statement).

Hivyo taarifa kuhusiana na mvua zinazoendelea imekuwa ikitolewa katika utabiri wa kila siku kupitia vyombo vya habari, mtandao wa kijamii wa Mamlaka na tovuti ya Mamlaka.

Tunawatakia shughuli njema katika ujenzi wa Taifa letu.

IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: