Msanii mahiri wa Kughani Mashairi kwa mtindo wa kisasa kabisa,Mrisho mpoto akizungumza mbele ya sehemu ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma na vitongoji vyake waliojitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya kamata Fursa twendzetu, iliofanyika ndani ya moja ya ukumbi wa hoteli ya  Africans dream, iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma. Semina ya Kamata Fursa twendzetu inayoratibiwa na Clouds Media Group, imekwishafanyika mikoa zaidi ya mitano ikiwemo  Kigoma, Tabora, Singida, Mtwara, Mbeya, Iringa sambamba na leo ndani ya Dodoma, ambapo semina hizo zote zimeonesha mafanikio makubwa kwa vijana kwali walikuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye ushiriki.
 Wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye semina hiyo ya kamata fursa twendzetu,mapema leo asubuhi mkoani Dodoma.
  Sehemu ya ya watu wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri kwenye semina hiyo.
 Meneja wa  NSSF mkoani Dodoma,Bwa.Kirondera Nyabuyenze akizungumza fursa mbalimbali zitokanazo na shirika la NSSF,Nyabuyenze amewataka watu mbalimbali wajitokeze kwa wingi kujiunga na NSSF,ili kujipatia fursa mbalimbali zikiwemo mikopo,matibabu na mambo mengiyo mbalimbali.
Mwakilishi wa Kampuni ya Maxmalipo,Renard Munuri akizungumza kwenye semina ya Kamata Fursa Twenzetu kwa vijana,kuhusiana na masuala mbalimbali yanayofanywa na kampuni yake katika kusaidia huduma za jamii,ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya  Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma.
 Mmoja wa Watangazaji mahiri wa Clouds FM, akizungumzia fursa mbalimbali alizokumbana nazo na namna alivyozifanyia kati na kujipatia sehemu ya  mafanikio katika kupambana na maisha.Semina ya Kamata Fursa twendzetu inayoratibiwa na Clouds Media Group, imekwishafanyika mikoa zaidi ya mitano ikiwemo  Kigoma, Tabora, Singida, Mtwara, Mbeya, Iringa sambamba na leo ndani ya Dodoma,ambao semina hizo zote zimeonesha mafanikio makubwa kwa vijana kwali walikuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye ushiriki.
 Sehemu ya wakazi wa mji wa Dodoma wakiwa wamejitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya fursa kwa vijana
 Sehemu ya meza kuu ya watoayo mada wakishangilia jambo.
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: