Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mwansiti Almasi,akifafanua namna
anavyonufaika na huduma za NSSF,mara tu walipojiunga kupitia kundi lao
la Lekadutigite,ndani ya semina ya fursa twendzetu iliyofanyika ndani ya
ukumbi wa Katema Hall,Midland hotel mkoani Morogoro mapema leo asubuhi.


Meneja huduma wa
Wajasiliamali-Zantel akizungumza mbele ya sehemu ya wakazi wa Morogoro
waliojitokeza kwenye semina ya Kamata fursa twendzetu,kuhusiana na fursa
mbalimbali zinazopatikana ndani ya kampuni hiyo,Semina hiyo iliofanyika ndani ya ukumbi wa Katema Hall,Midland
hotel mkoani Morogoro mapema leo asubuhi iliwakutanisha wadau mbalimbali.Semina
ya kamata fursa twendzetu inaratabiwa na Clouds Media Group,ambapo kwa sasa
imekwishafanyika ndani ya mikoa zaidi ya nane,ikiwemo Kigoma,Singida,Tabora,Dodoma,Mtwara,Mbeya,Morogoro
pamoja na Iringa.


wakifuatilia 
Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji, Ruge Mutahaba akifunga semina ya Fursa kwa vijana iliyofanyika mapema leo mkoani Morogoro.

 Semina ikiendelea ndani ya ukumbi . 
 Niki
wa Pili akielezea fursa mbalimbali wanazoweza kuzitumia vijana katika
nafasi mbalimbali wanazozipata,badala ya kubweteka na kusubiri fursa
ziwafuate hapo walipo,na pia amewataka vijana wenzake waache kulalama
kila kukicha na kuona maisha ni magumu,badala yake wanapaswa kujituma
kwa kila nafasi waipatayo.
 Sehemu ya meza kuu ikifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa na wadau ukumbini humo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya MaxMalipo,Bwana Ahmed Lussapi akizungumzia fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye kampuni yake,na pia namna ya kunufaika
nalo,amesema kuwa kwa sasa kampuni hiyo imekuwa ikiisaidia jamii katika
wigo mpana kwa kutoa huduma mbalimbali, hivyo amewataka vijana
kuchangamkia fursa za namna hiyo ili kujikwamua na ugumu wa maisha.
 Mbunifu
wa mavazi kutoka mkoani Morogoro,ambaye pia ni mjasiliamali
aliyejitambulisha kwa jina la Diana Magessa akionesha mbele ya washiriki
wa semina ya Fursa kwa Vijana (hawapo pichani) baadhi nguo zake
alizozidizaini kwa ubunifu wake.
 Mrisho Mpoto akisisitiza jambo.
 Mkali
wa kughani Mashairi,Mrisho Mpoto akizungumza na wakazi wa Morogoro
waliojitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya fursa twendzetu ndani
ya ndani ya ukumbi wa Katema Hall,Midland hotel mkoani Morogoro mapema
leo asubuhi
 Baadhi ya wageni waliohudhuria semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinajadiliwa ukumbini humo.
 Mmoja wa wasanii kutoka kundi la Weusi, Niki wa Pili akizungumza mbele ya
wakazi wa Morogoro wakati wa semina ya Fusra kwa vijana ikiendelea
ndani ya ukumbi wa Katema Hall,Midland hotel mkoani Morogoro mapema leo
asubuhi.Semina ya kamata fursa twendzetu inaratabiwa na Clouds Media
Group,ambapo kwa sasa imekwishafanyika ndani ya mikoa zaidi ya nane, ikiwemo  Kigoma,Singida,Tabora,Dodoma,Mtwara,Mbeya,Morogoro pamoja
na Iringa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: