Mhe. Harrison Mwakyembe alipotembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Tanzania House, Washington DC. Katikati ni Mhe. Waziri Harrison Mwakyembe akiwa na ujumbe wake akiwa na baadhi ya maofisa wa Ubalozi huo Bw. Paul Mwafongo (wa tatu Kushoto) na Bw.Suleiman Saleh (wa tatu kulia).
Mhe. Harrison Mwakyembe(Mb.)Waziri wa Uchukuzi akipokewa na mwenyeji wake Bw.Robert Shumake,Balozi wa Heshima wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Michigan mara baada ya kuwasili hotelini alikofikia.
Mhe.Waziri Mwakyembe katika picha ya pamoja na Bw. Shumake na Bw. Suleiman Saleh,Afisa wa Ubalozi wa Tanzania ,Washington DC.
Juu na chini ni Mhe. Mwakyembe katika taswira mbali mbali na Bw. Joelson, Mmiliki wa kituo cha kufundisha Urubani cha DCT katika ziara yake kituoni hapo ambapo alionyeshwa ndege za aina mbali mbali pamoja na kupata historia ya kituo hicho.
Mhe. Harrison Mwakyembe (katikati) na Ujumbe wake Bw. Peter Lupatu , Mkurugenzi wa Huduma za Usafiri,Wizara ya Uchukuzi, Bw.Suleiman Saleh Afisa wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC, Eng.K . Kisamfu, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli la Tanzania, Bw. Mohamed Millanga, Mkurugenzi wa Mradi (Terminal 3 Building), na Bw. Andrew Magombana katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya General Electric ya Erie, Pennsylvania.

Na Mwandishi wetu, Washington, DC
Mheshimiwa Dk.Harrison Mwakyembe(Mb.),Waziri wa Uchukuzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya ziara ya kikazi nchini Marekani katika miji ya Washington DC, Erie, Pennsylvania na Detroit, Michigan, kuanzia tarehe 18 -22 Septemba, 2013, kwa mwaliko wa Bw. Robert Shumake, Balozi wa Heshima wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika jimbo la Michigan. Wakati wa ziara hiyo, Mhe.Mwakyembe ambaye alifuatana na Bw. Lupatu, Mkurugenzi wa Huduma za Usafirishaji katika Wizara ya Uchukuzi, Eng. K. Kisamfu, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli la Tanzania, Bw. Mohamed Millanga,Mkurugenzi wa Mradi, Terminal Building 3, na Bw. Andrew Magombana,

Msaidizi wa Waziri. Mhe.Mwakyembe alipata fursa ya kutembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Washington DC na kisha kusafiri hadi Erie,Pennsylvania, kufanya mazungumzo na uongozi wa Juu wa kampuni ya General Electric inayotengeneza injini za treni.

Katika mkutano wake huo Mhe.Mwakyembe na ujumbe wake ulipata fursa ya kuelezwa shughuli mbali mbali za kampuni hiyo pamoja na kutembelea karakana kuu ya kampuni hiyo yenye watumishi zaidi ya laki tatu. Akiwa mjini Erie, Mhe.Mwakyembe alipata fursa ya kueleza mikakati iliyopo ya kuliboresha Shirika la Reli la Tanzania pamoja na kujenga mashirikiano zaidi baina ya kampuni na Serikali ya Tanzania katika kukamilisha azma hiyo.

Baadae Mhe. Mwakyembe na ujumbe wake ulisafiri hadi katika mji wa Detroit,Michigan, ambapo alipokelewa na alifanya mazungumzo na Bw.Shumake,Balozi wa Heshima wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye makazi yake katika mji wa Detroit.

Akiwa mjini humo Mhe. Mwakyembe alitembelea kituo cha mafunzo ya Urubani ambapo alielezwa historia ya kituo hicho pamoja namna ambayo kituo hicho kitasadia katika kuanzisha kituo cha Mafunzo ya Urubani nchini Tanzania. Aidha Mhe.Mwakyembe alipata wasaa wa kuonyeshwa aina ya ndege mbali zinazotumika katika mafunzo hayo. Kituo hicho kimetoa mafunzo mafunzo kwa marubani 3500 tangu kianzishwe miaka kumi na nane iliyopita.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: