Na Alex Kassuwi wa Swahili TV na Swahili Radio Online

Wiki iliyopita baada ya kulemewa  na maswali kutoka kwa wasomaji,wasikilizaji, watazamaji na wafuatiliaji wa vyombo vyetu vya habari vya MMK MEDIA GROUP watu wengi sana walituuliza  "kwa nini Swahili TV na Radio hawakuwepo katika tukio kubwa la kihistoria lililofanyika jumatano ya sept 18, 2013 katika ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani, ambapo Mabalozi wa Heshima (Honorary Consuls) walisaini mikataba mbele ya Rais wetu Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete. 
UKWELI NI KWAMBA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI UNABAGUA VYOMBO VYA HABARI AU AFISA  HABARI WAKE MINDI KASIGA

Baada ya tukio hafla hiyo kubwa kupita bila kusita  niliandika masikitiko yangu kwa niaba ya MMK MEDIA GROUP wamiliki wa Swahili TV online, Swahili Radio Online na Blog hii ya Swahilitv.blogspot.com kuhusiana na yaliyojitokeza ubalozini.
Leo hii katika tahariri hii nitaelezea na kufafanua makosa yaliyofanywa na  Ubalozi ama Mindi Kasiga na kwa nini hakupaswa ama hawakupaswa kubagua vyombo vya habari katika tukio lile. 

PIA NIMEAMBATANISHA BARUA YA MAMALIKO TOKA KATIKA CHOMBO KINGINE CHA HABARI KWA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI.

HIVI NDIVYO WAANDISHI TULIVYOTENDWA
Mosi; Mindi alionyesha dharau kwa kuwasiliana na vyombo vya habari kwa ujumbe mfupi wa email kutokea kwenye iPad yake katika akaunti yake binafsi ya gmail na badala ya kuandika barua ya kiofisi yenye nembo husika na yenye kumbukumbu na sahihi husika kama ilivyo kawaida. Kuthibitisha kwamba ni dharau, Mindi Kasiga alionyesha heshima pekee kwa shirika la  habari la kimarekani  VOA (Voice of America) kwa kuwapelekea barua ya kiofisi ya kuwaalika rasmi iliyozingatia taratibu zote za na sheria za kiofisi.
Pili; Mindi alisingizia ufinyu wa nafasi kuwa mdogo kwa vyombo vingine vya habari na huku mwaliko wa VOA ukiwa wazi kwa idadi ya watu wowote wale watakaopenda na watakaotaka kuhudhuria hafla ile wote walikaribishwa bila masharti.
Tatu; Mindi hakupaswa kujiamulia kwa kusema namnukuu "upande wa electronic media wote mtawakilishwa na jamii production". Swali 1. kwa Mindi hivi unaelewa nini kuhusu electronic media? au bado umebaki na mtazamo wa zamani ambapo kulikuwa na print na electronic iliyomaanisha Radio na TV ambavyo vilikuwa analojia, na tena terrestrial zikirusha matangazo kwa minara na mikonga ya mawasiliano. Swali 2. je, vipi kuhusu digital media? blogs, Online TV, Online Radio na Websites? hujui kwamba ndio vyombo vya habari vya leo vyenye wasomaji na wafuatiliaji wengi? Swali 3. Ni Criteria gani Ubalozi ama Mindi Kasiga waliyotumia kuiteua Jamii Production kuwakilisha vyombo vingine vya habari katika tukio la Kitaifa?

Nne; Mindi hukupaswa kuagiza vyombo vya habari vingine vipeleke maswali kwa Jamii production. Nakunukuu

"kama kuna maswali yaelekezwe kwao" Mindi huwezi kuagiza chombo cha habari kupeleka maswali yake kwa chombo kingine, kisha kile kingine kwenda kuuliza na kuleta majibu, hii haipo katika dunia ya sasa labda karne zilizopita. Jiulize ni kama vile Ikulu wana hafla halafu unaagiza TBC Taifa wapeleke maswali yao ITV halafu ITV wakaulize na kisha kuwaletea jibu TBC Taifa! uliona wapi hiyo?



BARUA YA MALALAMIKO TOKA KWA MWANDISHI MWINGINE AMBAYO ILITUMWA APRIL 2013 KWENDA UBALOZINI

Na Mubelwa Bandio
Shikamoo Mama Munanka.
Natumai kuwa u-mwema na unaendelea vema na kazi za kila siku hapo ofisini.
Binafsi ni mwema na naendelea na pilika za maisha hapa.
Napenda kutumia nafasi hii kueleza masikitiko yangu kidogo kuhusu hali ninayoona ikitokea kati ya ubalozi na jamii kwa ujumla.
Ntajaribu kufupisha jambo hili linalonisumbua sana
Nimekuwa mmoja wa wanaoletewa maswali ya “kwanini hamjazungumza na viongozi waliokuja hapo ubalozini” na kwangu nimepata wakati mgumu hata kufikiria jibu.
NI KWA KUWA HATA MIMI HUJIULIZA SWALI HILO
Nilishawahi kuleta maelezo na hata maoni ya namna ya kusaidiana na ubalozi kuunganisha jamii yetu hapa.
Binafsi naamini kuwa HAITATOKEA HATA SIKU MOJA, KUKAWA NA UJIO WA WAZIRI AMA RAIS AMA KIONGOZI YEYOTE WA NCHI KWA DHUMUNI MOJA TU LA KUKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO MAREKANI.
Ina maana, pale wanapopata ziara za kikazi, ndio wakati muafaka wa kukutana na / ama kuwasiliana nasi waTanzania tuishio huku (kama alivyofanya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe.)
SOTE TUNAJUA HILI SI KAWAIDA
Nilipata kuleta WAZO hapo ubalozini kuwa inapotokea ikajulikana kuna Mheshimiwa anayekuja, waTanzania katika DIASPORA waelezwe na waweze kutuma maoni kwa mhusika wa habari hapo ubalozini (kwa njia ya barua pepe), na mheshimiwa akija, tujumuishe maswali ya wanaDIASPORA na yale yatakayoandaliwa na wadau wa habari na kufanya mazungumzo nao.
Hii ingekuwa NJIA RAHISI NA MUAFAKA ya kuwasilisha mawazo, maswali na hata dukuduku la mTanzania wa Marekani popote alipo.
Lakini badala yake, tumekuwa tukisikia kuwa “walikuwepo” na / ama kuwaona katika MATUKIO na kisha wanaondoka.
Katika hili, NAONA KAMA UBALOZI UMETUANGUSHA KATIKA KUTUUNGANISHA NA WALE WANAOTUONGOZA.
Naamini mjadala na kiongozi toka Tanzania (iwe ni Townhall meeting ama mahojiano yanayoratibiwa na ubalozi) ni muhimu kwa jamii yetu
Nina hakika kuwa mikutano ya viongozi wanaokuja wanapokutana na viongozi wa Jumuiya na / ama vyama haikidhi mahitaji ya waTanzania wote nchini kwa kuwa wanakutana na viongozi wa Metropolitan waliyopo nao hawakutani na wanachama wote (hata wenye nia).
Nimeona niwasilishe wazo langu hili kwa mara ya mwisho nikiamini kuwa utawekwa utaratibu muafaka wa kuTUMIA VEMA ZIARA HIZI kuweza “kuua ndege wawili kwa jiwe moja”
Yaani, ndani ya ziara zao za kikazi, waunganishwe nasi watanzania tulio huku.
Natanguliza shukrani

NB: Nimewaambatanisha wanahabari wenzangu wa hapa DMV.
Chanzo:www.changamotoyetu.blogspot.com



mwisho wa barua ya Bandio
NAMALIZIA KWA HILI MUHIMU


Pamoja na mamaliko ya Mwandishi mwenzetu Mubelwa Bandio bado Ubalozi au Afisa habari wake hawajajirekebisha na bado kero ziko palepale na vyombo vya habari.

Swali, kwa nini viongozi wa kiserikali wanapokuja katika ziara za kikazi hapa nchini Marekani Ubalozi hautoi taarifa kwa vyombo vya habari? na badala yake Ubalozi unatumia chanzo kimoja cha habari, ambapo mwanahabari mmoja huyo anatumika ku-brake news za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati sisi wanahabari wengine tunastukizwa na habari za ujio wa viongozi walifika lini, wamefanya nini nk toka katika chombo hiki kimoja na tunabaki tukijiuliza hiki ni chombo binafsi ama kitengo cha Ubalozi? Tungependa kuwe na Freedom of Speech, na Ushirikishwaji kwa vyombo vya habari vyote bila kubagua. Vyombo vya habari vipo na vinajulikana na Ubalozi unavitambua kwani vilishajitambulisha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: