Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera Akiwasili Kwenye Uwanja wa Shujaa Mkoani morogoro Akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mh Said Amanzi Wakati  wa hafla fupi ya kumpongeza Bondia Francis Cheka aliyeiletea sifa nchi kwa kushinda ubingwa wa dunia kwa Kwa kumchapa  bingwa wa dunia Mmarekani Bondia Phills Williams  Cheka amezawadiwa kiwanja  mabati, na Tani moja ya saruji
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera Akimpokea Bondia Francis Cheka wakati akiwasili uwanjani  katika halfa ya kumpongeza Bondia huyo aliyenyakua Ubingwa wa Dunia Kwa Kumchapa bondia kutoka Marekani.


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera Akikabidhiwa Mkanda wa Ubingwa wa Dunia kutoka kwa Bondia Francis Cheka Mjini Morogoro

Bondia Francis Cheka akitoa neno la Shukrani na Pembeni yake Ni Mke wa Bondia Huyo
Mkuu wa wilaya ya Mvomero na rais wa Riadha Tanzania Mh Antony Mtaka Akisema machache
Akizungumza katika hafla Mkuu wa Mkoa Mh Joel  Bendera alisema  ushindi wa Cheka ni sifa kwa tanzania katika  mchezo wa ngumi. Bondia Francis Cheka amezawadiwa kiwanja  mabati, na Tani moja ya saruji.Picha na MATUKIO NA MICHAPO BLOG
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: