Watumishi wa Mungu Christina Shusho na Upendo Kilahiro, mwishoni mwa wiki hii watahudumu katika jiji la Washington DC na Vitongoji vyake (DMV).

Shusho na Kilahiro ambao ni miongoni mwa waimbaji mahiri wa muziki wa Injili Afrika Mashariki, wameshawasili Washington DC tayari kwa huduma hiyo ambayo ni sehemu siku tatu za Maadhimisho ya miaka mitano ya kanisa la The Way Of The Cross Gospel Ministries.

Maadhimisho haya yataanza siku ya Ijumaa na kumalizika Jumapili

Maadhimisho haya yatafanyika:-
The Way of the Cross Gospel Ministries
(at University United Methodist Church)
3621 Campus Drive
College Park, MD 20740

Hii inakuwa ni mara ya pili kwa watumishi hawa kuhudumu pamoja kanisani hapo katika kipindi cha miaka miwili, ambapo mwaka 2011 waliungana na Upendo Nkone kuhudumu katika Mkutano mkubwa wa Injili ulilofanyika kanisani hapo.

Watazame na kuwasikiliza wanavyoelezea siku hizo...

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: