Wageni waalikwa wakiwa katika sherehe ya kutolewa mahari kwa binti Myoma Kapya iliyofanyika nyumbani kwa Mbezi beach jijini Dar es Salaam.
 Mzee David Kapya (kulia) ambaye ni baba yake mzazi Myoma Kapya (Nadine) akipokea shuka la babu kutoka kwa Mchungaji Jomalema ambaye ni mmoja ya wazazi wa Kijana Mussa Saidi ikiwa ni moja ya mahari ya binti yake.
  Mzee David Kapya (kulia) ambaye ni baba yake mzazi Myoma Kapya (Nadine) na Mchungaji Jomalema (kushoto) wakimsikiliza mshenga wakati akisoma vitu walivyokuwa wameagizwa.
  Mzee David Kapya ambaye ni baba yake mzazi Myoma Kapya (Nadine) akipokea Majembe kutoka kwa Mchungaji Jomalema ambaye ni mmoja ya wazazi wa Kijana Mussa Saidi ikiwa ni moja ya mahari ya binti yake.
 Wajomba nao wakikabithiwa mbuzi zao.
  Bwana harusi mtarajiwa Mussa Saidi akijiandaa kumvalisha pete ya uchumba, Myoma Kapya (Nadine).
 Bwana harusi mtarajiwa Mussa Saidi akimvalisha pete ya uchumba, Myoma Kapya (Nadine).
 Baba mzazi akiwapongeza vijana wao na kumkaribisha rasmi nyumbani kwake kijana wake.
 Mama mzazi wa Myoma Kapya (Nadine) akiwapongeza.
 Watarajiwa wakiwa katika nyuso za furaha.
Mambo hayo ya pete ya uchumba.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: