Serikali imesimisha kwa muda machimbo ya Moramu yaliyoko katika Kata ya Moshono Jijini Arusha baada ya kusababisha vifo vya watu 13 na kujeruhi 2 ili kuweza kufanya tathmini ya kimazingira mazingira ya machimbo hayo kwa kuwa ni muhimu kwa shughuli za ujenzi wa mkoa hapa.
Uamuzi huo wa Serikali umeelezwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akihudhuria ibada maaalum ya ya pamoja kuaga miili ya marehem waliokufa katika machimbo hayo kwa kufukiwa na kifusi, zoezi lililofuatiwa na kuzuru eneo la ajali na kujionea hali halisi.
Mh Pinda pia aliwatembelea majeruhi waliolazwa hospitali ya Mt Meru na pia kuwapa pole wafiwa.
Akiwa katika eneo la ajali, Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi kuwa hawajafunga machimbo hayo moja kwa moja bali yamesitishwa kwa muda kwa ili kuboresha mazingira ya machimbo hayo katika kuepusha hatari nyingine, kutokana na umuhimu wake katika ujenzi pamoja na kipato kwa wananchi..
Jumla ya maiti 13 wanatarajiwa kuzikwa kwesho katika makaburi ya nyumbani kwa wafiwa.
Kwa mujibu wa taarifa ilizozifikia Kajunason Blog zilisema kuwa Ibada itafanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Moshono Dayosisi ya Kaskazini, Usharika wa Mara na baadae kuaga na kila ndugu kuchukua maiti zao kwenda kuzika katika makaburi yao ya boma.
Toa Maoni Yako:
0 comments: