Kijana fundi  seremala ambae  pia alichonga  jeneza la marehemu Bw Solomon a.k.a Baba akiliweka wakifu kaburi kwa kulimwangia mchanga ambao  yeye alidai ni maji ya uzima.
 Baadhi ya  waombolezaji  wa msiba  huo  wakiwa  wamekata tamaa baada ya katekista  kuingia mitini leo.
 Hapa mhubiri  wa kujitolea akiongoza ibada ya mazishi kwa kutoa neno.
 Mwili  wa marehemu Rejina Lweve  ukiwa makaburini



Baadhi  ya  waombolezaji  wa msiba  wa Bi Rejina  Lweve mkazi  wa  Kihesa katika Manispaa ya  Iringa wameeleza kusikitishwa kwao na udanganyifu uliofanywa na mmoja kati ya makatekista  wa RC eneo la Mgongo  baada ya mtumishi huyo wa Mungu kudaiwa kutumia lugha ya udanganyifu kukwepa kuongoza idaba ya mazishi kwa madai  kuwa anakwenda kutafuta maji ya uzima.


Tukio  hilo lilionyesha kuwakwaza zaidi waombolezaji hao na kupelekea baadhi yao kuamua kuondoka kabla ya shughuli za mazishi kufanyika.


Wakizungumza na mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com baadhi ya  waombolezaji  walisema  kuwa hawajapendezwa na hatua ya  kiongozi huyo  wa kidini  kususia  kuongoza  ibada  hiyo na  kuwa kufanya hivyo ni  kushusha  heshima la kanisa hilo la RC ambalo  linaheshimika  zaidi duniani .


Hivyo  wamemwomba askofu wa kanisa  hilo mkoani Iringa  kulitazama kwa kina  suala  hilo ili ikiwezekana  kuwaondoa watendaji kazi wa parokia na vigango ambao  wanatabia kama  hizo za  kusisia maiti.


Pia walisema kuwa kateksta huyo aliaga  kuwa anakwenda kufuata maji ya uzima  nyumbani kwake ila toka alipoondoka mida ya saa 8 hakuweza kurejea tena hadi saa 10 jioni  walipoamua kumtuma dereva wa  boda boda  kumfuata  bila mafanikio na kulazimika kumwomba mchonga majeneza Kihesa ili  kuendesha idaba hiyo. 
 
SHUKRANI ZA DHATI: Francisgodwin Blog. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: