TUKIO LA AJALI YA MAPOROMOKO YA MORAMU ILIYOSABABISHA VIFO VYA WATU KUMI NA TATU
Mnamo tarehe 01/04/2013 muda wa saa 4:40 asubuhi huko moshono Tanganyika Parkers kwenye machimbo ya moramu, watu kumi na tano (15) wakiwa katika uchimbaji na upakiaji wa moramu waliangukiwa na kifusi cha udongo wa moramu na hatimaye kusababisha vifo vya watu kumi na tatu (13) na wawili kujeruhiwa.
Taarifa hizo zinaeleza kwamba, muda wa saa 4:00 asubuhi watu hao walikuwa wanapakia moramu katika magari mawili ambayo ni scania lenye namba za usajili T. 886 BDA na jingine ni aina ya mitsubishi fuso lenye namba za usajili T. 109 AYB.
Ilipofika muda huo wa asubuhi, kifusi cha moramu kiliporomoka ghafla na kuwafunika watu wote waliokuwa katika eneo hilo. Mpaka hivi sasa Jeshi la Polisi mkoani hapa limetambua miili ya marehemu pamoja na majeruhi. Waliofariki katika ajali hiyo ni:- Julius s/o Peter Palangyo (56) mkazi wa Nkoaranga wilayani Arumeru, Fredy s/o Loserian (21) mkazi wa Tanganyika parkers moshono, Christopher s/o Laurent (24) kondakta na ni mkazi wa Kijenge, Gerald s/o Jacob maarufu kwa jina la Kababu (24) mkazi wa moivaro, Gerald s/o Masai (33) mkazi wa Tanganyika Parkers, Japhet s/o Amani Kivuyo (27) mkazi wa Moshono na Mwenda s/o Stephano (25) mkazi wa moivaro.
Wengine ni Elias s/o Fanuel (28) mkazi wa Tanganyika Parkers, Barick s/o Kipara (26) mkazi wa moshono, Seurii s/o Raphael maarufu kwa jina la mbu (24) mkazi wa moshono, Alex s/o Marick (23) dereva na ni mkazi wa moshono, Hassan s/o Mussa (24) mkazi wa moshono na wa mwisho ni Gerald s/o Nerujangi (45) mkazi wa moshono.
Majeruhi katika ajali hiyo ni samwel s/o Gunda (29) kondakta, mkazi wa moshono na Mariaki s/o Lenanu (48) mkazi wa Tanganyika Parkers ambao wote walikuwa wamelazwa katika hospitali ya Mount Meru hiyo jana na Samwel s/o Gunda amesharuhusiwa huku mwenzake akiendelea kupatiwa matibabu. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mount meru. Asanteni kwa kunisikiliza.
Imetolewa na Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,
Kamishna msaidizi wa polisi,
(ACP) Ibrahim Kilongo
Tarehe 02/04/2013
Toa Maoni Yako:
0 comments: